JUMLA ya shilingi milioni 50,363.400 zimetolewa kama mkopo usiokuwa na riba kwa vikundi 32 vya vijana,wanawake na walemavu katika Halmashauri ya wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma.

Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Tunduru Gasper Balyomi alisema, lengo la mikopo hiyo kuyawezesha makundi hayo kiuchumi ili yaweze kukuza miradi,kuhimarisha vikundi na kutoa nafuu kwa wanavikundi namna Bora ya kufanya shughuli zao bila bughuza.

Balyomi alisema, mkopo huo kwa vikundi hivyo pia ni utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2015-2020 inayotaka kila Halmashauri hapa nchini kutenga na kutoa asilimia 10 ya mapato ya ndani kusaidia makundi maalum .

Kwa mujibu Balyomi, hii ni mara ya pili kwa Halmashauri kutoa mikopo kwa vikundi mwaka 2019 ambapo Mwezi Februari walitoa shilingi milioni 33.500.000 kwa vikundi 10 vya vijana,10 wanawake na vikundi 4 vya walemavu.

Aidha,amewahasa wana vikundi kubuni miradi iliyo na faida na ya kiushindani kutokana na utandawazi uliopo kwa sasa kwa kutengeneza na kuzalisha bidhaa zitakazokuwa na ushindani na wazalishaji wengine kwani uzoefu unaonesha kuwa baadhi ya vikundi vlivyopo katika wilaya hiyo uzalisha bidhaa duni na zisizo na ubora katika soko.

Balyomi, amewataka kuepuka kuanzisha miradi wasiokuwa na uzoefu nayo kwani inaweza kuwagharimu wakati wa marejesho,bali kuanzisha miradi yenye faida watkaomudu kurejesha mkopo kwa wakati ili watu wengine nao wapate fursa ya kukopeshwa.

Amewaomba wataalam wa fani mbalimbali kuwasaidia wana vikundi katika kuendesha miradi kwa miradi ya vikundi vingi hufa na kukosa uendelevu kutokana na wataalam kuwa mbali na wana vikundi husika.

Amewaagiza maafisa wa idara ya maendeleo ya jamii kwenda kuwasaidia wana vikundi jinsi ya kuendesha miradi kusudi kama vile miradi ya kilimo na mifugo ambayo inahitaji ukaribu wa wataalam ili ilete faida na kumudu kurejesho mkopo kwa muda muafaka.

Pia amewaelekeza wataalam wa idara mbalimbali katika halmashauri kuvisaidia vikundi kutafuta fursa nyingine za uwezeshaji badala ya kutegemea halmashauri pekee kama ufungaji nyuki ambavyo vitaunganishwa na wakala wa misitu(TFS) ili viwezeshwe fedha za uendeshaji wa miradi.

Awali Afisa maendeleo ya jamii Halmashauri ya wilaya Tunduru Fadhil Chidyaonga amewaomba wananchi kuitumia fursa hiyo kujiunga katika vikundi vya uzalishaji mali vya vijana,wanawake na walemavu.

Alisema, kumekuwa na chagizo la vikundi vinavyo bahatika kukopeshwa na Halmashauri kutoridhika na kuona mkopo wanaoupata kuwa mdogo kilinganishwa na mahitaji ya mradi husika.

Mmoja wa wana kikundi hao Fatuma Mtesa alisema, mikopo hiyo itawasaidia kuendeleza shughuli zao na kuongeza uzalishaji wa bidhaa ili kujikwamua na umaskini.

Hata hivyo,ameiomba Serikali kuongeza kiwango cha mkopo ili waweze kuanzisha miradi mikubwa ambayo itawapatia faida kubwa na kufanya mambo mengi ya maendeleo kama kujenga nyumba bora.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...