Na Mwandishi Maalum; Mbulu 

Wakulima Wilayani Mbulu wameiomba serikali iwapelekee wataalamu wa kilimo na pembejeo za kutosha ili kuwawezesha kuwa na kilimo chenye tija zaidi. 

Ombi hilo lilitolewa na umoja wa Wamwagiliaji wa Skimu ya umwagiliaji ya Mangisa iliyopo katika kata ya Dongpbeshi, Wilayani Mbulu Mkoani Manyara walipokuwa wakiongea na waandishi wa habari na wataalamu kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji jana walipoitembelea skimu hiyo. 

Akizungumza kwa niaba ya umoja wa Wamwagiliaji katibu wa umoja huo Damiano Sulle alisema serikali kwa kushirikiana na wafadhili ilifanya jambo la msingi kuleta skimu ya umwagiliaji katika eneo hilo ambapo ameeleza kuwa imeleta tija kwani ndio ajira pekee iliyo badilisha maisha ya wakazi wengi katika kata ya Dongobeshii. 

“Kabla ya kuwepo kwa skimu hii mkulima aliweza kuvuna chini ya gunia kumi (10) kwa tani au kumi na tano (15) za kitunguu saumu kwa hekta na baada ya kuboreshwa kwa miundombiu ya kisasa ya umwagiliaji mkulima anaweza kupata hata gunia hamsini (50) ya zao hio kwa hekta” Alisema Bwana Sulle. 

Sulle ameiomba serikali kuwasaidia kusakafia mfereji ambao haujasakafiwa wenye urefu wa mita 50 ambao utawasaidia wakulima kujipanga vizuri hasa katika matumizi sahihi ya maji na kuongeza uzalishaji zaidi wa mazao. 

Sambamba na hilo wakulima wameomba serikali kuwatafutia soko la uhakika hususan la zao la kitunguu swaumu ili waweze kuuza zao hilo kwa mfumo wa stakabadhi ya mazao ghalani kwani wana maghala makubwa ya kutosha ambapo wangeweza kuhifadhi mazao hayo na kuuyauza wakati ambao bei za mazao hayo zikiwa juu. 

Wilaya hiyo ya Mbulu ina eneo la Hekta 2400 zinazofaa kwa kilimo cha umwagiliaji na hekta 1250 ndizo zinazotumika kwa kilimo hicho ambapo kuna skimu saba ambazo ni Mangisa, Dongobeshi,Tumati,Diyomati,Dirm, Ari na Bashay skimu ambazo zinatumika kwa kilimo cha zao la mahindi, Viazi, Shayiri na mazao mengine ya mbogamboga.
 Moja ya mfereji unaopeleka maji katika mashamba ya mazao ya mboga mboga na mahindi katika skimu ya Mangisa iliyopo wilayani Mbulu Mkoani Manyara.
 sehemu ya miundombinu iliyojengwa na Serikali kupitika shirika la kimataifa  la maendeleo laJapan JICA chini ya uasimamizi wa Tume ya Taifa ya uwagiliaji  katika skimu ya kilimo cha umwagiliaji Mangisa inayopokea maji kutoka kwenye mabwawa kupeleka katika mashamba ya mazao mbalimbali
 shamba linaloonyesha zao la kitunguu swaum zao ambalo limekuwa likiwangizia wakulima kipato kikubwa katika skimu ya umwagiliaji Mangisa iliyopo Wilayani Mbulu Mkoani Manyara.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...