Meneja wa Tigo Kanda ya Kaskazini Lilian Mwalongo (kati kati) akikabidhi sehemu ya miavuli 200 kwa viongozi wa wafanya biashara wadogo wadogo mkoani Arusha maarufu kama Wamachinga. Kulian ni mwenyekiti wa umoja huo Amina Njoka na kushoto ni makamu mwenyekiti Iddi Hussein

Meneja wa Tigo Kanda ya Kaskazini Lilian Mwalongo (kati kati) akikabidhi moja ya boksi lenye simu 247 kwa viongozi wa wafanya biashara wadogo wadogo mkoani Arusha maarufu kama Wamachinga. Kulian ni mwenyekiti wa umoja huo Amina Njoka na kushoto ni makamu mwenyekiti Iddi Hussein.

Meneja wa Tigo Kanda ya Kaskazini Lilian Mwalongo (kati kati) akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi kabla ya kukabidhi zawadi za simu 247 kwa viongozi wa wafanya biashara wadogo wadogo mkoani Arusha maarufu kama Wamachinga. Kulian ni mwenyekiti wa umoja huo Amina Njoka.
Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya Tigo mkoani Arusha wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa wafanyabiashara wadogo wadogo maarufu kama Wamachinga muda mfupi bada ya kuwakabidhi simu 247 pamoja na miavuli 200 kwa ajili ya kusaidia kuboresha biashara zao jijini Arusha jana.



Kupitia Chama Cha Wamachinga Mkoa wa Arusha, leo tarehe 26/06/2019 kampuni ya Tigo kupiti kitengo chake cha Tigo Business imetoa simu 247 pamoja wa miavuli 100 kwa wateja wake ambao ni wanachama wa umoja huo wa wafanya biashara wadogo wadogo.

Akizungumza wakati wa hafla fupi ya kuwakabidi vifaa hivyo kwa wateja hao 247, Meneja wa Tigo Kanda ya Kaskazini Lilian Mwalongo alisema, zawadi hizo ni utaratibu wa kawaida wa kampuni hiyo kuwazawadia na kuwashukuru wateja wake waliopo kwenye vikundi na unalenga kuboresha biashara zao pamoja na mazingira wanayofanyia kazi.

“Leo kampuni ya Tigo inayofuraha kukabidhi vifaa hivi kwa wateja wetu ambao ni wanachama wa Umoja wa Wamachinga hapa mkoani Arusha. Ni utaratibu wetu wa kawaida kuwapa zawadi wateja waaminifu kama hawa na tunaamini vifaa hivi vitawasadia kuboresha biashara zao huku wakifurahia huduma bora kutoka Tigo,” alisema

Lilian alifafanua kuwa, kampuni ya Tigo hutoa zawadi mbali mbali ikiwamo simu za mkononi kwa wateja wa malipo ya baada waliopo kwenye vikundi na ambao hutumia huduma za Tigo wakiwa na mkataba wa miezi 12 au 24.

Ili mteja aweze kunufaika na zawadi hizi anatakiwa kujiandikisha kama mteja wa walipo ya baada (postpaid) na ni lazima awe katika kikundi au kampuni kubwa AU ndogo. Hivyo basi, tunakaribisha vikundi, makampuni pamoja na taasisi kwa ajili ya kupata huduma zetu nzuri na za uhakika za mawasiliano.

Meneja huyo pia aliwataka wanafuaika wa zawadi hizo kuendelea kutumia mtandao wa Tigo na kuongeza kuwa Tigo inajali na kuwekeza kwa wateja na wabia wake wa biashara ili kuhakikisha kuwa watanzania wote wawanufaika na huduma bora za mawasiliano.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...