Na Dominick Salamba
Zimebaki siku chake kabla ya Fainal za mataifa ya Afrika zianze nchini Misri na miongoni mwa mataifa machache ambayo yamepata bahati ya kushiriki katika michuano hiyo ni Taifa letu pendwa la Tanzania..

Imepita takribani miaka 39 tukiwa washuhudiaji wa michuano hii kwa kuangalia mataifa ya wenzetu na kufikia hatua ya kujibatiza ushabiki wa kudumu kwa baadhi ya nchi masalani wapo ambao wanasema wao ni mashabiki wa Nigeria,Cameron,Ghana,Misri,Senagal na mengine mengi hii yote ilitokana na kitendo cha kua mashabiki wa mda mrefu kwa kushuhudia mataifa mengine yakishiriki..

Wakati wetu umefika na nitakua mchoyo wa fadhila kama sito pongeza juhudi za Serikali yetu,Tff,na wadau mbalimbali ambao walisimama kidete kwa nguvu,hali na mali hili tu kuona tunaingia kwenye historia ya soka la Afrika kwa mara nyingine..

Shukrani za pekee kama sio maalumu lazima nizitoe kwa benchi la ufundi likiongozwa na Emanuel Amunike na Wachezaji wote walioshiriki kuanzia mwanzo wa kuitafuta nafasi hii na kweli wakafanikisha hili..

Katika mchakato huu toka mwanzo wametumika wachezaji wengi hati imefika mahali imepatikana Timu ya wachezaji 23 ambao ndio watatuwakilisha kwenye michuano hiyo tukiwa kwenye kundi moja na Senagal,Algeria na majirani zetu Kenya na katika hao wachezaji 23 wapo 11 ambao ndio watatufungulia pazia katika mechi ya ufunguzi na kutoa picha kamili ya soka letu..

Nirejee nyuma kidogo kwanini imenisukuma kuandika waraka huu sababu moja kubwa ni kutokana na maneno mengi ambayo yameibuka na kupewa nafasi bila kujua madhara yake na ni kinyume na matamanio yetu kwani kila mtu amekua mwalimu kila mtu amekua na kikosi chake kila mtu amekua na mipango yake kuhusu namna ya timu inatakiwa iwe na wachezaji gani watumike,Si dhambi kutoa maoni lakini tukumbuke kua maoni na ushauri ni ziada sio kitu halisi na uamuzi wa wale wanaoshauriwa na tumekwenda mbali mpaka kuanza kutaja majina ya wachezaji ambao tunaona hawafai kuwepo na wanaofaa wakati timu imeshatangazwa hii si sawa tena si sawa..

Tukumbuke kua soka ni taaluma tena taaluma kamili mbinu na mikakati inapangwa na jopo la benchi la ufundi na mtazamo wao ndio silaha yetu kuu na maneno ya dhihaka tunayoyasambaza juu ya timu yetu hayawachafui tunaowataja bali tunajichafua wenyewe ni sawa kutoka nje na kueleza madhaifu ya mzazi wako kwa watu wengine..

Tumeanza kuikataa Timu yetu kabla ya michuano kuanza hivi wakifanya vema kule tutafanyeje tutaendelea kua hivi hadi lini?

Ifike mahali tuheshimu taaluma na sio kila jambo ni lazima kutafuta ubaya hata pasipo na sababu mbona wenzetu hawana haya,timu imekwenda inahitaji sapoti yetu kubwa na kama kuna marekebisho baada ya mashindano kuna jopo ambalo litatoa tathimini ya mashindano yote mapungufu na nini tufanye katika michuano ijayo..

Tujue kuwa kuna idadi maalumu hata tungekua na wakina messi na ronaldo 50 wanaotakiwa ni 23 tu kwa mujibu wa mahitaji ya mwalimu kulingana na mbinu halizoziandaa..

Mwalimu yupo na timu kambini anakaa na wachezaji anajua mienendo na mtazamo wao juu ya michuano husika inafika mahali anatangaza kikosi cha mwisho unaibuka kutoka sijui Vikindu unaanza kwanini kamuacha fulani wakati anauwezo hivi unadhani mchezaji ni uwezo tu?kuna tofauti kati ya mchezaji na timu unaweza kua mchezaji mzuri ila ukashindwa kutengeneza timu nzuri..

Tuachane na kujimaliza wenyewe tujikite katika kuwatia moyo wa ujasiri tuzungumze mazuri yao tuoneshe tunawaamini na tupo nyuma yao waone upendo na shauku zetu juu ya uwajibikaji wao ndio njia nzuri ya kuwatia shime kinyume na hapo inaonesha kua basi hatuka na nia ya dhati kuona tunashiriki..

Ombi langu mitandao ya kijamii,waandishi wa habari,wachambuzi,walimu,na,wadau wengine tutumie vinywa vyetu,kalamu zetu na chochote tukitumiacho kuona tunaandika mazuri ya Timu yetu tuache chuki na kutafuta umaarufu binafsi kwa kutumia njia hasi ili tujizolee umaarufu kwa urahis hapana hili swala la kitaifa linawaunganisha Watanzania popote pale walipo..

Timu ni yetu na tuiamini na wanaweza kutupatia furaha na naimani watafanya vizuri kwa kadri ya uwezo wao wote tuanze wote ili tumalize wote kama Taifa..
Asante...@dominicksalamba

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...