*Baraza lahaidi kuendeleza ushirikiano ili kuipeleka sanaa mbali zaidi

Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii.
BARAZA la sanaa nchini (BASATA) kupitia bodi ya sanaa wamekutana na wasanii kutoka kada mbalimbali na kujadili changamoto na namna ya kuzitatua ili kuweza kuipeleka mbele tasnia hiyo ambayo inachangia pato la taifa kwa asilimia 13.5.

Akizungumza katika kikao kazi hicho katibu mtendaji mkuu wa BASATA Godfrey Mwingereza amesema kuwa baraza hilo linaendelea kutatua changamoto zinazowakumba wasanii hasa katika kuhakikisha haki zao kutoka kwa kile wanachokifanya zinazingatiwa.

Amesema kuwa ushirikiano baina ya baraza hilo na wasanii kutoka mashirikisho mbalimbali ndio daraja linalounganisha wasanii na baraza hilo na kujadili changamoto wanazokumbana nazo katika kazi wanazozifanya.

Aidha amewataka wasanii hao  kuwa mabalozi bora katika jamii hasa kwa kuenzi tamaduni, kuvaa mavazi yenye staha, kudumisha lugha ya Kiswahili, kutotumia na kuelimisha jamii kutotumia dawa ya kulevya kupitia kazi zao na kufanya kazi za  mkataba zinazitambulika na baraza hilo.

Kwa upande wake mwenyekiti wa bodi hiyo  Habbi Gunze amesema kuwa baraza hilo linashirikiana na mashirikisho yote manne ya wasanii ambayo ni wasanii wa filamu, sanaa za maonesho, sanaa za ufundi na Muziki katikabkuhakikisha sanaa inakua na kwenda mbali zaidi.

Amesema kuwa sanaa ni kama kazi nyingine ambazo zinawaingizia vijana kipato na inachangia pato la taifa kwa asilimia 13.5 hivyo ni vyema wasanii na wadau wakashirikana katika kuijenga sanaa ambayo kwa namna moja au nyingine inatambulisha taifa.

Gunze  amewataka wasanii kuwa na ushirikiano na kufanya kazi zao kwa kuzingatia maadili pamoja na kuyatumia mashirikisho kuwasilisha kero zao ili ziweze kutatuliwa kwa wakati.

Baadhi ya washiriki wa kikao kazi hicho wameshukuru baraza la sanaa la taifa kupitia bodi hiyo kwa kuitisha kikao hicho na kushauri kuwe na utaratibu wa kukutana na wasanii hao ili kuipeleka sanaa mbele zaidi pamoja na kuweka mfumo wa kutoa mafao pindi wanapokutana na majanga mbalimbali na pindi wanapoufikia uzee.

Katibu mtendaji mkuu wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Godfrey Mwingereza akizungumza na wasanii na wadau wa filamu waliojitokeza katika mkutano huo ambapo amewahakikishia wasanii kuwa baraza hilo litaendelea kushirikiana nao hasa katika kutatua changamoto zinazoikumba tasnia nzima ya sanaa, leo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti ya Bodi ya Sanaa nchini Habbi Gunze akizungumza na wasanii na wadau wa filamu ambapo amewataka kufanya kazi kwa bidii na kwa kuzingatia maadili, leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wasanii na wadau wa sanaa waliohudhuria mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa baraza la sanaa nchini (BASATA) leo jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...