Na Woinde Shizza Michuzi Tv,Arusha

Shirika la umeme nchini (Tanesco)Kanda ya kaskazini limesema kuwa Wateja wakubwa wa Umeme nchini (wawekezaji wa viwanda)wamekuwa muhimili mkubwa kwa shirika hilo kwa sababu wanachangia kwa kiasi kikubwa mapato ya shirika hilo kwa asilimia zaidi ya 40.

Akizungumza kwenye Semina ya wadau na wawekezaji wa viwanda kanda ya kaskazini Mkurugenzi wa Kanda ya Kaskazini wa shirika hilo mhandisi Stella Hizza amesema kuwa japo wadau hao ni wachache lakini wamekuwa ni mhimili mkubwa wa mapato ya shirika.

Amesema kuwa Uwepo wa wateja wakubwa na wenye viwanda ndio wanachangia shirika hilo kuweza kutoa huduma bora za uhakika ndio maana wameanzisha kitengo maalum cha kuwapatia huduma stahiki kutokana na mchango wao wa maendeleo ya shirikia na nchi.

Kwa Upande wake Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amesema kuwa Mkoa wa Arusha unawakaribisha Tanesco kuwekeza miundombinu ya umeme kwenye eneo la malula lenye ukubwa wa ekari 500 ambalo litajengwa bandari kavu ili kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji.

Amesema eneo hilo linasifa zote hivyo kuweka mazingira mazuri ya kushawishi uwekezaji katika eneo hilo kwa kuwa reli inapita katika eneo hilo na kuwataka wafanyabiashara hao kuona fursa ya kuchangamkia uwekezaji katika mkoa wa Arusha.

Nae Mzalishaji wa umeme mdogo kutoka kijiji cha kwa Sadala mkoani Kilimanjaro Thomas Munuo anayezalisha umeme wa jua Kv 40 amelitaka shirika hilo kuwatembelea na kuwatambua wadau hao wanaozalisha umeme ili kuweza kushirikiana nao kwa lengo la kuleta maendeleo kwa wananchi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...