Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina (wa tatu kushoto) akitoa tuzo kwa Mshindi wa kwanza wa Fahali bora kutoka Mbozi, Mkoani Iringa, Abraham Mwalutende wakati wa maonesho ya  Ng`ombe Bora wa Maziwa yaliyofanyika katika Viwanja vya Nanenane jijini Dodoma juzi.Wapili Kushoto ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Kimataifa  ya Utafiti wa Mifugo (ILRI), Dk. Jimmy Smith na Kutoka kulia ni Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega.
 Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina (kushoto), akisalimiana na  Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI), Dk. Eligy Shirima alipokwenda kufungua rasmi Maonesho ya  Ng`ombe Bora wa Maziwa Tanzania yaliyofanyika katika viwanja vya Nanenane, Nzuguni jijini Dodoma jana. Katikati ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Kimataifa  ya Utafiti wa Mifugo (IRLI), Dk. Jimmy Smith.

 Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof. Elisante Ole Gabriel (wa pili kulia) akizungumza wakati wa  maonesho ya  Ng`ombe Bora wa Maziwa yaliyofanyika katika Viwanja vya Nanenane jijini Dodoma juzi. Wengine kutoka kulia ni, Mkurugenzi wa Taasisi ya Kimataifa  ya Utafiti wa Mifugo (ILRI), Dk. Jimmy Smith;  Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI), Dk. Eligy Shirima na Msimamizi wa Mradi wa Utafiti wa Vinasaba vya Ng`ombe wa Maziwa kutoka Taasisi ya Kimataifa  ya Utafiti wa Mifugo (ILRI), Dk.Okeyo Mwai.

 Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina (katikati) akitoa tuzo kwa Mshindi wa kwanza wa ng`ombe bora wa maziwa kutoka Meru, Mkoani Arusha, Emmanuel Nanyaro wakati wa maonesho ya  Ng`ombe Bora wa Maziwa yaliyofanyika katika Viwanja vya Nanenane jijini Dodoma juzi.Kushoto ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Kimataifa  ya Utafiti wa Mifugo (ILRI), Dk. Jimmy Smith.
 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega (kushoto), akihutubia wakati wa uzinduzi wa maonesho ya Ng’ombe bora wa maziwa yaliyoandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) kwa kushirikiana na Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa  Mifugo (ILRI) pamoja na wadau kutoka maeneo mbalimbali katika Viwanja vya NaneNane Mkoani Dodoma juzi.
 Mkurugenzi wa Taasisi ya Kimataifa  ya Utafiti wa Mifugo (ILRI), Dk. Jimmy Smith (kushoto), akihutubia wakati wa uzinduzi wa maonesho ya Ng’ombe bora wa maziwa yaliyoandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) kwa kushirikiana na Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa  Mifugo (ILRI) pamoja na wadau kutoka maeneo mbalimbali katika Viwanja vya NaneNane Mkoani Dodoma juzi.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI), Dk. Eligy Shirima akizungumza katika hafla hiyo.

Na Ripota wa Michuzi TV
WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina amezitaka Taasisi za Utafiti wa Mifugo nchini kuhakikisha wanafanya tafiti zaidi nchini Tanzania kwa lengo la kubaini ng'ombe bora wa maziwa zilizpo ikiwa ni makakati wa kuongeza upatikanaji wa maziwa nchini. 

Ameweka wazi kwa sasa Tanzania kuna ng'ombe wa maziwa milioni 1,294,882 na uzalishaji wa maziwa ni lita bilioni 2.7 kwa mwaka wakati mahitaji ni lita bilioni 11, hivyo kuna upungufu wa maziwa lita bilioni 7.3 kwa mwaka. 

Mpina ameeleza hayo wakati wa Moanesho ya Ng'ombe Bora wa Maziwa nchini Tanzania ambayo yamefanyika kwa mara ya kwanza katika Viwanja vya Nanenane Mjini Dodoma na kuhudhuria na wadau wa sekta ya maziwa kutoka ndani na nje ya nchi ikiwemo Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Mifugo . 

Akifafanua zaidi kwenye maoesho hayo, Waziri Mpina amesema Tanzania ni ya pili kwa kuwa na idadi kubwa ya mifugo ikongozwa na Ethiopia barani Afrika lakini unapozungumzia sekta ya uzalishaji maziwa iko chini ukilinganisha na nchi nyingine za Afrika Mashariki. 

"Kwa mwaka Tanzania kwa upande wa maziwa yanayosindikwa ni lita milioni 70 wakati hapa majirani zetu wa Kenya kwa mwaka wanazalisha maziwa ya kusindikwa lita milioni lita zaidi ya 800. 

"Kwa mwaka tunaagiza maziwa yaliyosindikwa kutoka nje ya nchi lita milioni 20 ambazo thamani yake ni Sh. bilioni 30 kwa ajili ya kuagiza maziwa wakati hapa nyumbani tuna ng'ombe wengi na hii ni aibu ambayo awamu ya Tano imeweka mkakati wa kuimaliza,"amesema Mpina. 

Pia amewataka Watanzania na hasa wadau wa ufugaji wa ng'ombe wa maziwa kuchangia fursa hiyo ya uhaba wa maziwa kwa kuzalisha kwa wingi na kwa upande wa Serikali imejipanga kuhakikisha sekta ya mifugo inaleta tija kwa Taifa. 

"Ukweli uliopo kwa idadi ya mifugo ambayo tunayo hapa nchini , hata hao ambao wanaonekana ni washindani wetu huenda sio washindani kabisa kwetu.Kwa mikakati ambayo Wizara yetu inayo na malengo ya Serikali ya Awamu ya Tano tunauhakika Tanzania tutakuwa wa kwanza kwa kuzalisha maziwa mengi na yaliyobora,"amesisitiza. 

Kuhusu jumbe ambazo zimetolewa wakati wa maonesho hayo , amekiri imezungumzia changamoto ya uhaba wa dawa za chanjo za mifugo na malisho ya mifugo,ambapo amesema Serikali imeshaweka mikakati kuondoa changamoto hizo pamoja na nyingine. 

Amesema Serikali itahakikisha dawa zinapatikana kwa gharama nafuu na sio bei ya juu ambayo wafugaji wanauziwa.Pia Wizara imejipanga kukabiliana na magonjwa ya mifugo na kufafanua kupitia maabara za mifugo zilizopo watahakikisha kabla mifugo haijaingia nchini inafanyiwa vipimo,kama sehemu ya kukabiliana na magonjwa ya mifugo. 

Wakati huo huo Waziri Mpina amesema Wizara imedhamiria kuhakikisha bei ya maziwa inaongezeka kwani bei ya sasa ni ndogo na binafsi anamia sana anapoona bei ya lita ya maziwa inakuwa chini ya Sh.1000. 

Akizungumzia ng'ombe bora wa maziwa , amesema kuna idadi kubwa ya ng'ombe hao na hivyo hakuna sababu ya kuagiza mbegu kutoka nje ya nchi na kwamba kupitia tafiti zinazoendelea katika vituo vya utafiti vilivyopo nchini na hasa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania kuna uwezekano wa kuwa na madume mengi zaidi yenye mbegu bora. 

"Nikiri yapo malalamiko makubwa kutoka kwa wananchi kuhusu madume ya ng'ombe aina ya Mtamba na tayari Wizara na Serikali kwa ujumla imeweka mikakati ya kuhakikisha tunakuwa na mitamba mingi zaidi .Hivyo taasisi zetu za utafiti zihakikishe zinafanya tafiti nyingi na katika mikoa mingi zaidi,"amesema. 

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Mifugo Tanzania Dk.Jimmy Smith pamoja na mambo mengine amesema anaishukuru Serikali ya Awamu kuwa kutoa nafasi kwa taasisi yake kushiriki katika kuongeza tija katika sekya ya ufugaji wa ngo'mbe wa maziwa. 

Pia amesema kupitia teknolojia ya mawasiliano wamekuwa wakikusanya taarifa za wafugaji pamoja na kufanya tafiti mbalimbali kwa kutumia vinasaba ambavyo vinachukuliwa kupitia manyoya ya ng'ombe na utafiti ambao wameufanya kwa ng'ombe 6000 , wamefanikiwa kupata waliobora 40. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...