WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema ni wakati muafaka kwa Watanzania kuanza kujiwekea akiba kwa kununua hisa kupitia taasisi za kifedha nchini ikiwemo benki ya CRDB.

Ametoa kauli hiyo leo (Jumapili, Juni 16, 2019) wakati wa bonanza kati ya Wabunge na watumishi wa benki ya CRDB lililofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

Waziri Mkuu amesema suala la wananchi kujiwekea akiba ni muhimu kwa ajili ya maendeleo yao. "Nashauri wananchi tutumie taasisi za fedha kujiwekea akiba pamoja na kukopa mikopo kwa ajili ya maendeleo yetu."

Akizungumzia kuhusu bonanza hilo lililoandaliwa na benki ya CRDB, Waziri Mkuu amesema michezo ni sehemu nzuri kujenga afya, furaha na kujenga mshikamano wa karibu baina ya benki hiyo na wananchi ambao ni wateja.

Michezo iliyochezwa katika bonanza hilo ni mpira wa miguu ambapo timu ya CRDB ilishinda baada ya kuifunga timu ya Bunge penati tatu kwa moja na kwa upande wa mchezo wa mpira wa pete timu ya Bunge iliibuka na ushindi baada ya kuibugiza CRDB magoli 35 kwa mawili.

Katika mchezo wa kuvuta kamba timu ya Wabunge Wanawake na Wanaume waliibuka na ushindi baada ya kuzishinda timu za CRDB. Upande wa mchezo wa basketball timu ya Bunge ilishinda vikapu 53 kwa 51.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
41193 - DODOMA.
JUMAPILI, JUNI 16, 2019.
Waziri Mkuu Mkuu,Kassim Majaliwa akimkabidhi nahodha wa Timu ya Soka ya Benki ya CRDB ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Abdulmajid Nsekela, kikombe cha ushindi wa mechi ya soka ya kirafiki kati ya timu hiyo na timu ya Bunge iliyochezwa kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma, Juni 16, 2019. CRDB ilishinda 3-1. 
Wachezaji na mashabiki wa timu ya soka ya benki ya CRDB wakishangilia baada ya kukabidhiwa kikombe cha ushindi baada ya kuitandika timu ya Bunge 3-1 katika mechi ya kirafiki ilichezwa kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma, Juni 16, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na mchezaji nyota wa timu ya mpira wa pete ya Bunge, Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Mama Salma Kikwete kabla ya kuanza kwa mechi ya kirafiki kati ya Bunge na CRDB iliyochezwa kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma Juni 16, 2019. Bunge ilishinda 35-2. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...