Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe amezindua rasmi kampeni maalumu ya kuchangia timu ya Taifa “Taifa Stars” inayoshiriki mashindano ya Kombe la Maifa ya Afrika (AFCON) yanayotarajiwa kuanza Juni 21 nchini Misri.
Waziri Mwakyembe amesema watanzania hawana budi kuchangia kiwango chochote na kwamba fedha hiyo itakuwa salama na itawafikia wachezaji hao bila ya mizengwe yoyote.

"Watanzania kote nchini wanaweza kuichangia timu yao  kupitia akaunti zifuatazo BMT N BC 011101000978, Sport Development Fund, CRDB 01J1019956700 na Voda *150*00#5595298. Ukichangia, ujumbe unaopata utume  kwenda 0735 414043 jina litakuja Oscar Zabloni ambye ni mweka hazina ,'' amesema Dkt. Mwakyembe.

Amesema wote watakaochangia watapewa cheti  maalumu na  kiongozi wa kitaifa ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wao katika kuhakikisha timu yetu ya Taifa inafanya vizuri katika mashindano hayo.

Naye mwenyekiti wa kamati ya kusaidia Taifa Stars, Paul Makonda amesema siku ya Jumamosi Juni 22, 2019 mkoa wa Dar es Salaam utafanya maombi maalum kwa ajili ya  kuiombea timu ya Taifa Stars ambayo inatarajia kushuka dimbani siku ya Jumapili Juni 22 dhidi ya timu ya Taifa ya Senegal.
Pamoja na mambo mengine Makonda amezitaka kampuni 41 zilizoahidi kuchangia Taifa Stars kutoa michango hiyo.

"Jumamosi ya Juni 22,2019 Mkoa wa Dar es Salaam tutafanya maombi maalum kuiombea timu ya Taifa Stars, na pia nitumie nafasi hii  kuyakumbusha  makampuni  yaliyoahidi kuichangia Taifa Stars sasa wachangie kupitia akaunti hizo,'' amesema Makonda.
Timu ya Taifa Stars iko kundi C, pamoja na timu za Senegal, Algeria na Kenya ambapo siku ya Jumapili inatarajia kutupa karata yake ya kwanza dhidi Senegal.

Tayari Stars imeshacheza mechi mbili za kirafiki za kujipima nguvu, huku ikipoteza mchezo wake wa kwanza dhidi ya Misri 1-0 na kutoka sare ya goli 1-1 dhidi ya Zimbabwe.
 Katibu wa Kamati ya kuisadia timu ya Taifa “Taifa Stars”, Mhandisi Hersi Said (kulia)  akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa harambee maalum ya kuichangia timu hiyo mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kushoto ni Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe na katikati ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Paul Makonda.
 Mwenyekiti wa Kamati ya kuisaidia timu ya Taifa “Taifa Stars”, Paul Mokonda akimkaribisha Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe wakati wa uzinduzi wa kampeni maalum ya kuichangia timu ya Taifa inayoshiriki mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) nchini Misri.
 Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe (wa pili kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya kampeni maalum ya kuichangia timu ya Taifa “Taifa Stars” inayoshiriki mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) nchini Misri.
 Mbunifu wa mavazi akionesha kwa waandishi wa habari vazi maalum kwa ajili ya washangiliaji wa timu ya Taifa “Taifa Stars”, inayoshiriki mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) nchini Misri.
 Mwenyekiti wa Kamati ya kuisaidia timu ya Taifa “Taifa Stars”, Paul Mokonda (katikati) akijaribu vazi maalum kwa ajili ya washangiliaji na mashabiki wa timu ya Taifa “Taifa Stars”, inayoshiriki mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) nchini Misri.
 baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia kwa makini uzinduzi wa kampeni maalum ya kuichangia timu ya Taifa “Taifa Stars” inayoshiriki mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) nchini Misri.
Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe (wa tatu toka kushoto) akimkabidhi cheti Mwenyekiti wa Kamati ya kuisaidia timu ya Taifa “Taifa Stars”, Paul Mokonda kwa kutambua mchango wake katika kufanikisha kufuzu kwa timu hiyo katika mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) nchini Misri.
Picha na WHUSM – Dar es Salaam.
17/06/2019


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...