Mmoja wawafanyakazi wa TCRA Arusha
akiendelea kutoa elimu kwa mwananchi
Na Woinde Shizza Michuzi TV, Arusha 
Zoezi la kusajili laini za simu kwa kutumia mfumo mpya wa alama za vidole umekua wa mafanikio makubwa Mkoani Arusha kwa mamia ya wananchi kujitokeza kwa wingi katika viwanja hivyo kujisajili kwa kutumia vitambulisho vya Taifa vya NIDA na alama za vidole
Zoezi ilo limeendeshwa na mamlaka ya mawasiliano Tazania TCRA kwa kushirikiana na maafisa wa NIDA pamoja na maafisa wa uhamiaji kwa lengo la wananchi kusajili laini zao pamoja na wengine kupata vitambulisho vya NIDA  kwa wale wasiokua navyo na kufanya zoezi ilo kuwa rahisi zaidi kwa wananchi
Akizungumzia zoezi ilo Mhandisi Imelda Salmu ambaye ni Kaimu Mkuu wa Mawasiliano  Kanda ya Kaskazini amesema zoezi ilo limeanza siku tatu zilizo pita wakianza na Chuo cha Uhasibu jijini Arusha na usajili huo kuwa na mafanikio makubwa na baadae kuingia katika viwanja vya soko la Kilombero
Kwa upande wao waratibu wa Nida  Julieti Raimondi alisema  lengo la kufika kwenye viwanja vya standi nikuwahamasisha wananchi wote ambao hawajawahi kujiandikisha waweze kufika  ili wafanikishe usajili wa simu zao na wale ambao bado awapata nao wanaangalia niwapi tarifazao zimekwama na waweze kuwatatulia matatizo yao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...