Na.Khadija seif, Michuzi tv

BARAZA la Sanaa la Taifa (BASATA) limewataka wasanii kufuata utaratibu wa kusajiliwa kwenye baraza hilo ili watambulike kwa mujibu wa sheria.

Hayo yamesema leo baada ya Wasanii Wa maigizo (Bongo Movie) Irene Uwoya na Steve Nyerere kutotambulika na BASATA kutokana na kushindwa kufuata utaratibu wa kisheria wa kusajiliwa.

Kaimu Katibu Mtendaji BASATA, Onesmo Kayanda amesema kuwa kwa sasa wasanii wengi wanafanya kazi zao za Sanaa bila ya kufuata taratibu za kujisajili.

"Wengi wanaingia katika sanaa bila utaratibu wanafanya kazi kwa ujanja ujanja mambo ya utandawazi pia yamekua yakichangia kutoona umuhimu wa kujisajili , badala yake linapotokea tatizo ndipo linapokuja swala la yeye kutotambulika na Basata,"

Kayanda amesema wasanii wengi wanafanya kazi zao bila kutambulika na mamlaka husika zaidi mitandao ya kijamii ndiyo inawatambua zaidi na anakua kinyume na kazi zake.

Aidha,Onesmo ameeeeza lengo la kuwaita wasanii hao wawili Irene uwoya pamoja na Steve Nyerere kufika Basata ni kufanya mazungumzo kuhusu mambo ya tansia ya sanaa na pamoja kupatiwa elimu,faida na hasara zitakazojitokeza endapo utakua unatambulika kisheria kama msanii kupitia Baraza la sanaa (BASATA).

" Tumezungumza mambo muhimu yanayohusu sanaa hichi ni kikao cha familia ndio kikubwa zaidi na tumegundua pia wao ni baadhi ya wasanii ambao hawajasajiliwa Basata na hawatambuliki kisheria.

Katibu huyo alifafanua Kitendo cha Msanii wa Bongomovie Irene Uwoya kudhalilisha waandishi katika Mkutano wa Kampuni ya kuuza filamu mtandaoni ya Swahiliflix kilichofanyika katika ukumbi wa Kilimanjaro hotel jijini Dar es salaam cha kuwarushia pesa wanandishi kwa dharau kuwa waandishi wasione limepuuzwa bali sio la kuliweka wazi sana kwa sasa.

"Tunatambua kuwa amefanya kosa sisi kama viongozi tunalifanyia kazi ila si lazima kuliweka wazi".

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...