Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akizungumza na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB), Alex Mubiru alipomtembelea ofisini kwake Jijini Dodoma.
Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB), Alex Mubiru (kulia) akielezea jambo wakati wa mazungumzo yake na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Phillip Mpango (Mb), Jijini Dodoma. 
Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB), Alex Mubiru akielezea jambo wakati wa mazungumzo yake na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Phillip Isdor Mpango (Mb) (hayupo pichani), Jijini Dodoma. 
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Adolf Ndunguru (kushoto), na Kaimu Kamishna wa Fedha za Nje Bw. Adrian Njau wakisikiliza kwa makini mazungumzo kati ya Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Bw. Alex Mubiru (hawapo pichani), kilichofanyika Jijini Dodoma. 
Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB), Alex Mubiru akielezea jambo wakati wa mazungumzo yake na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Phillip Mpango (Mb), Jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto) akiwa na mgeni wake Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB), Bw. Alex Mubiru aliomtembelea na kufanya naye mazungumzo katika Ofisi Ndogo ya Hazina-Treasury Squire, Jijini Dodoma. 
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Phillip Mpango (Mb), akiteta jambo na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB), Alex Mubiru (kulia) mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Jijini Dodoma. 
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Phillip Mpango (Mb) (aliyeketi mbele kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB), Alex Mubiru (kulia) mara baada ya kumaliza mazungumzo yao jijini Dodoma. Waliosimama wa pili kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Bw. Adolf Ndunguru wa Wizara ya Fedha na Mipango na Maafisa wengine waandamizi kutoka Wizara hiyo. 
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Phillip Mpango (Mb) (kushoto), akiagana na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB), Bw. Alex Mubiru (kulia) mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Jijini Dodoma. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini- Wizara ya Fedha na MIpango) 

……………………….. 

Na Saidina Msangi na Josephine Majura, WFM, Dodoma 
Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) inatarajia kuipandisha daraja Tanzania kutoka katika hadhi ya kunufaika na Mfuko wa Maendeleo wa Benki (ADF) hadi kuwa na hadhi itakayoiwezesha Tanzania kuweza kupata rasilimali fedha zaidi kupitia dirisha la African Development Bank (ADB) la Benki ya Maendeleo ya Afrika. 

Endapo Tanzania itafanikiwa kupandishwa hadhi, nchi itaweza kunufaika na ongezeko la fedha kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika kutoka Dola za Marekani milioni 350 kwa mwaka hadi Dola za Marekani milioni 812 kwa mwaka. 

Hayo yamesemwa Jijini Dodoma na Mwakilishi Mkazi wa Benki hiyo Dr. Alex Mubiru alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango, katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha na Mipango-Treasury Square. 

Katika mazungumzo hayo, Dr. Alex ameeleza kuwa hatua hiyo ya kupandishwa hadhi ama kupandishwa daraja inatokana na uchumi wa nchi kufanya vizuri hususani katika maeneo ya kasi ya ukuaji wa uchumi na kuwa na deni himilivu. 

“Hatua hiyo itaiwezesha Tanzania kupata fedha zaidi kutoka katika Benki hiyo na kuwezesha utekelezaji wa miradi ya maendeleo na vipaumble kwa Serikali” Alisisitiza Bw. Mubiru. 

Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB), Bw. Alex Mubiru, amesema kuwa benki hiyo inajivunia kufanya kazi na Tanzania ambayo ni miongoni mwa nchi Waasisi wa Benki hiyo. 

Katika mazungumzo yao, Dkt. Mpango ameeleza kuwa Serikali inajivunia kufanya kazi pamoja na Benki ya AfDB kwa kuwa benki hiyo imekuwa na masharti rafiki katika upatikanaji wa mikopo. 

Dkt. Mpango amesema kuwa Benki hiyo ina mtazamo chanya katika maendeleo ya watu na kuwa dira katika mipango ya maendeleo na kuahidi kushirikiana nao vyema katika kukuza uchumi wa nchi. 

Aidha, Waziri Mpango ameipongeza benki hiyo kwa kukubali kutekeleza miradi ya Ujenzi wa Barabara ya Mzunguko Dodoma (km110.2) kwa kiwango cha lami pamoja na ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Dodoma (Msalato) na kubainisha kuwa uamuzi huo ni mzuri kwani licha ya Dodoma kuwa ni Makao Makuu ya nchi lakini pia miundombinu hii itaunganisha na kuchochea ukuaji wa uchumi na biashara katika mikoa mingi nchini pamoja na nchi jirani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...