Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii 

Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) imezindua Shindano la Masoko ya Mitaji kwa Wanafunzi wa Vikuu pamoja na Taasisi za Elimu ya Juu kwa mwaka 2019.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa Uzinduzi huo Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) Nicodemus Mkama amesema Shindano hilo ni kuwajengea uwezo wa Wanafunzi wa elimu ya juu kuwajengea uwezo katika Masoko ya Mitaji ikiwa ni pamoja kufanya sekta hiyo kutambulika na watanzania.

Amesema uzinduzi huo ni sehemu ya utekelezaji wa mpango mkakati wa mamlaka wa miaka mitano 2018/2019 hadi 2020/ 2023 ikwa ni dhamira ya serikali kuendeleza sekta ya Masoko na Mitaji kwa kutoa elimu kwa makundi mbalimbali.

Mkama amesema mkakati mwingine ni kuongeza uelewa na ushiriki katika Masoko ya Mitaji kwa lengo la kupanua wigo kwa wsshiriki hao kujenga uwezo wa watendaji katika sekta hiyo.

Afisa Mtendaji Mkuu huyo amesema mamlaka inatekeleza mikakati kwa njia mbalimbali ikiwa pamoja na kutoa elimu kwa Umma na kwa makundi mengine akiwemo Shindano kwa ajili ya wanafunzi wa elimu ya juu hapa nchini.

Wawekezaji na wsshiriki wa Shindano katika Masoko ya Mitaji wanahitaji kupata uelewa wa kutosha kuhusu Masoko ya Mitaji na namna ya kushiriki hatua umuhimu ya kuwawezesha kulinda masilahi yao na kufanya uwekezaji huo kuwa endelevu.

Amesema elimu ya Masoko ya Mitaji inawezesha pia kundi la Wanafunzi kuepuka kushiriki fursa za uwekezaji za kitapeli na udanganyifu ambapo siku za usoni kumekuwa na wimbi kwa vijana kulagaiwa na kushiriki.

Mkama amesema tangu waaze mashindano kumekuwa na mwitikio kwa wanafunzi wa Vyuo kushiriki.Amesema 2015/2016 washiriki walitaka 2000 lakini walipata washiriki 7,500 na 2016/2017 lengo ilikuwa 7000 wakapata washiriki 7,901,2017/2018 lengo lake ilikuwa 10,000 wakapata 15,004 na mwaka huu ni kupata washiriki 16,000.

Amesema washindi watapelekwa katika nchi mbalimbali katika kujifunza namna wanavyoendesha sekta hiyo.
 Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) Nicodemus Mkama akizungumza wakati uzinduzi wa Masoko ya Mitaji kwa Wanafunzi wa Vyuo Vikuu   pamoja na Taasisi za Elimu ya Juu nchini lilofanyika katika mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam.
 Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na Shindano la Wanafunzi wa Vyuo Vikuu na Taasisi za Elimu ya Juu lilofanyika katika mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam.
 Mwanafunzi wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Adela Niko akizungumza namna alivyojipanga katika kushiriki Shindano la Masoko ya Mitaji
Mwanafunzi wa Chuo Kikuu Huria Dustan Komba akitoa matarajio yake katika Shindano la Masoko ya Mitaji

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...