Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Sarah Msafiri akizungumza na wananchi wa mtaa wa Kizani kata ya Gezaulole alipofika kutoa pole na kuzungumza na wananchi hao, na amewataka wananchi  kuwa makini na kuishi kwa tahadhari leo jijini Dar es Salaam.
Wananchi wa kata ya Gezaulole waliojitokeza katika kikao hicho, leo jijini Dar es Salaam.
 Nyumba iliyofanyika tukio la mauaji na kuchomwa moto kwa bi. Naomi Orest Marijani huko Gezaulole Kigamboni jijini Dar es Salaam.

*Awataka wananchi kuhoji matatizo ya ndugu na watu wao wa karibu na kutoruhusu kukumbatia matatizo.

Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
TUKIO la kupotea kwa bi. Naomi Orest Marijani au Sandra (36) na baadaye kugundulika ameuawa, kuchomwa moto na kuzikwa na mume wake Khamis Ruwongo (38), wananchi wa mtaa wa Kizani kata ya Gezaulole Wilaya ya Kigamboni wametakiwa kuchukua tukio hilo kama funzo na kuwa makini kwa kutoyakumbatia matatizo yao hasa ya kifamilia.

Akizungumza na wananchi wa mtaa wa Kizani kata ya Gezaulole Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Sarah Msafiri ameeleza kusikitishwa na tukio la kupotea kwa Naomi na baadaye kugundulika ameuwawa na mume wake.

Sarah amesema kuwa haki itatendeka na kuonekana na kuwaasa wananchi hasa vijana kudhibiti  siasa zisizo na msingi na kuelekeza matukio hayo kwa wanaowaita watu wasiojulikana.

Pia amewashukuru sana ndugu wa Naomi kwa ushirikiano wao wa kutoa taarifa zilizosaidia katika uchunguzi na kuwaomba viongozi wa dini kutumia majukwaa ya dini katika kuhimiza amani na upendo katika familia.

Amesema kuwa vyombo vya ulinzi vinaendelea na uchunguzi na tukio hilo ambalo si la kuigwa na si la kitanzania na wala sio tukio la kujifunza kabisa.

Amesema vyombo vya ulinzi vimelaani vikali tukio hilo na kuwahakikishia wananchi kuwa serikali ya awamu ya tano ipo makini na kila afanyaye tukio la namna hiyo kwa namna yoyote ile atafahamika na kueleza kuwa matukio yoyote ya kiharifu yanayosukwa kokote yatamulikwa kwa kuwa vyombo vya ulinzi vipo makini.

Aidha amesema kuwa Kama Kuna mitandao inayoshiriki katika kufanya hayo, ambapo amekemea vikali na kusema kuwa hayo yote yatafika mwisho na amewaomba wananchi kutoa ushirikiano katika tukioh hilo na ya namna hiyo. 

Na amewashauri wanawake kutokumbatia matatizo ya kifamilia pamoja  na kutodharau mambo wanayosikia kwa majirani na watu wao wa karibu na tukio hilo liwe fundisho na kuishi kwa tahadhari.

Kwa upande wake diwani wa kata ya Kizani amesema kuwa msiba huo ni mkubwa na wanaishukuru serikali, Waziri wa mambo ya nje na mkuu wa Wilaya kwa ushirikiano hadi tukio hilo likafikia kwenye hatua hiyo.

Vilevile Katibu tawala wa Wilaya ya Kigamboni Rahel Mhando ametoa pole na kuelezwa kusikitishwa na tukio hilo la kusikitishwa na kusema kutumia wasaa huo kueleza kuwa uchaguzi wa serikali za mitaa unakaribia na kuwashauri wanakijii kuchagua watu sahihi watakaoweza kuwatumikia wananchi.

Amesema kuwa tarehe 23 mwezi mtaa wa Kinzani utapitiwa na Mwenge wa uhuru kwa kufungua mradi wa maji na kuwataka wananchi wa Kinzani kujitokeza kwa wingi ili kuweza kufurahia huduma ya maji kwa mitaa mitatu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...