Anaandika Abdullatif Yunus wa Michuzi TV.

Kutokana na kushindwa kukamilika kwa wakati mradi wa Maji safi na salama kwa Wakazi wa Eneo la Murongo Wilayani Kyerwa Mkoani Kagera, Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa Mhe. Rashid Mwaimu amelazimika kumsweka ndani Meneja wa Kampuni ya CSR ambao ndio wanaotekelezaji Mradi wa Maji unaotokana na Mradi Mkubwa wa kufua umeme wa Kikagati - Murongo (Kikagati/Murongo Hydro power Project).

Kufuatia hali hiyo Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa Rashid Mwaimu amemuagiza Mkuu wa Kituo cha Polisi Kyerwa kumshikilia na kumuweka chini ya uangalizi kwa muda wa wiki mbili Meneja wa Masoko wa Kampuni ya CSR , Alice Bachuta (34), ambae pia ndiye aliyesaini mkataba, ambapo kwa muda wote huo Kandarasi huyo anatakiwa kufanya linalowezekana kupatikana Maji, au kurudisha hela yote zaidi ya Shilingi Milioni 26 ambayo ni malipo ya awali.

Imebainika kuwa licha ya kandarasi huyo kupewa zabuni hiyo, utendaji kazi wake umekuwa dhaifu kiasi cha kusogeza mbele muda wa kazi zaidi ya Mara mbili, akiomba aongezewe muda wa kukamilisha mradi huo (extension of time), licha ya awali kudai angemaliza kazi yote ndani ya mwezi mmoja. 

Mkandarasi huyo CSR kutoka Jijini Mwanza ameshindwa kukamilisha kwa wakati mradi huo Mkubwa wa kuchimba kisima cha Maji, wenye kugharimu zaidi ya Shilingi Milioni Hamsini na Tatu, ikiwa tayari 50% ya pesa yote imeshalipwa Kwa Mkandarasi huyo na Maji yameshindikana kupatikana, makubaliano yakiwa ni kupatikana Maji ndani ya mwezi mmoja toka Mwezi wa Tatu, mpaka sasa Mwezi wa saba, na kwa kazi yote imefanyika 30% tu.


 Pichani Meneja Masoko kutoka CSR Drilling Co Ltd. Akipanda gari la Polisi kuelekea Kituoni kwa hatua nyingine baada ya DC Mwaimu kuelekeza hivyo.
 Pichani DC Rashid Mwaimu akitoa maelekezo ya kushikiliwa kwa Alice Bachuta (hayupo pichani) mpaka Mradi wa Maji ukamilike vinginevyo atalazimika kurudisha pesa ya awali aliyopewa.
 Pichani ni Alice Bachuta Meneja Masoko na mwakilishi wa Kampuni ya CSR Drilling Co ltd, ambaye pia ndiye aliyesaini mkataba na kupewa kiasi cha pesa Milioni 26 ili kutekeleza Mradi wa Maji Murongo, akiwa ofisini kwa DC Kyerwa akitoa Maelezo yake.
 Kikao Cha Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa Mhe. Rashid Mwaimu kikiwa kimeketi kujadili kero ya Maji na kushindwa kukamilika kwa Mradi wa Maji wa unaotokana na Mradi mkubwa wa Kikagati - Murongo.
 Pichani Gari lenye Mtambo wa Kuchimba Visima virefu la Kampuni ya CSR Drilling Co. Ltd likiwa limetelekezwa kwa muda wa Miezi miwili na Mkandarsi, huku hatma ya Mradi wa Maji kwa wakazi ikiwa haifahamiki.
 Pichani Ni bomba lenye urefu wa Mita Tisa likiwa limezamishwa ardhini sehemu kinapochimbwa kisima, licha ya uhitaji wa bomba hilo ni Mita 100, na hiki ndicho kimefanyika mpaka sasa ingawa Mkandarasi ameshalipwa Milioni 26.
 Pichani ni Eneo unapotekelezwa Mradi wa Maji kwa wakazi wa Murongo, ambapo Mkandarasi Kampuni ya CSR Drilling Co. Ltd ya Jijini Mwanza imeshindwa kukamilisha kazi hiyo kwa wakati.
Pichani ni Binti Mkazi wa Murongo Yasintha John akiteka maji ya kutumia kutoka Mto Kagera kwa ajili ya matumizi ya Nyumbani kama alivyokutwa na Kamera yetu.

 Pichani ni Maji ya Mto Kagera yanayotumiwa na wakazi wa Murongo Wilayani Kyerwa, ambao mpaka sasa wameshindwa kupata Maji safi na salama kutokana na Mkandarasi kushindwa kukamilisha Mradi wa Maji Eneo hilo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...