Na Woinde Shizza, Michuzi Tv,Arusha 

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro amefurahishwa na kazi zinazofanywa na Chuo cha Uhasibu Arusha,amekiomba chuo hicho kuendelea kuwaandaa vijana kitaaluma na kivitendo ili kuja kupambana katika changamoto ya soko la ajira. 

Muro liyasema hayo chuoni hapo wakati akifunga maonyesho ya nadharia na vitendo ya kitaaluma yaliyoshirikisha shule 18 za sekondari mkoani hapa ambapo alitumia Muda huo kukipongeza na kukisifu chuo hicho kwa kutoa elimu mbalimbali pia kuwahamasisha vijana waliopo kidato cha nne kusoma kwa bidii ili waweze kufaulu na kujiunga na elimu ya chuo .

Aidha alifafanua kuwa chuo hicho kimefanya ubunifu mkubwa wa kushirikisha vijana wa sekondari za mkoa wa Arusha kuona kazi mbalimbali zinazofanywa na chuo hicho kwani kwakufanya hivyo wanawaandaa Vijana hao wa sekondari kwa ajili ya kujiunga na elimu ya vyuo vikuu kwa baadaye. 

"Hapa kuna wanasayansi, uchumi, watu wa mapambo na upishi wa keki hii yote ni lengo la chuo kuwawezesha vijana ili wakimaliza masomo wasitoke na elimu ya darasani tu bali kwenda kuwa wajasiriamali ili waendeshe maisha yao. "alifafanua Muro

Alitumia mda huo kuwahasa wanafunzi hao kuwa makini katika swala zima la kusoma na kutilia manani masomo kwani katika soko la ajira la kipindi hiki ili uweze kushinda nalo lazima uwe na elimu ya kutosha ya natharia na vitendo. 

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo hicho Profesa Eliamani Sedoyeka Alisema kuwa chuo hicho kitaendelea kutoa elimu bora ili kuwawezesha wanafunzi kuwa na ujuzi wa kuendesha maisha yao baada ya masomo. 

"Kila kozi anayosoma mwanafunzi anapewa kazi mbalimbali ili ajue kwa vitendo kwani lengo letu nikutoa wajasiriamali pia huko waendako wakaweze kupata ajira na kujiajiri kwani soko la ajira kwa sasa ni changamoto kubwa "aliongeza Profesa Sedoyeka. 

Aidha alitumia nafasi hiyo kuwaacha vijana wao au watoto wao kuchagua masomo ambayo wanayataka wenyewe kuyachukua na sio kuwachagulia kombi,aliwataka wazazi kuwapeleka watoto wao chuoni hapo kwaajili ya kujifunza mambo mbalimbali yanayoendana na soko la Ajira. 

"chuoni kwetu pia tunatoa ushauri ni masomo gani mwanafunzi achukue ili aendane na soko la ajira iwe anataka kuajiriwa au anataka kujiajiri hivyo wazazi walete watoto wao ili wapatiwe ushauri mzuri"alifafanua Profesa Sedoyeka

Kwa upande wake mmoja ya mwanafunzi alieshiriki maonyesho Hayo Bundalla Bachia kushukuru na kusema maonyesho hayo yamewasaidia kwani yanawapa fursa ya kujifunza kivitendo masomo wanayofundishwa darasani

Alibainisha kuwa maonyesho hayo yamewatengenezea uzoefu na ujuzi kwani wamekutana na wanachuo wanaosoma fani mbalimbali hivyo wanatarajia kujiunga nazo mara baada ya kidato cha nne na hiyo inawapa hamasa ya kufikia Elimu ya juu.
Mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro katikati akimkabithi kapteni wa timu ya mpira wa miguu kutoka Shule ya sekondari mara baada ya kushinda katika michezo iliyoandaliwa na Chuo cha uhasibu Arusha,wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Chuo hicho Profesa Eliamani Sedoyeka .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...