Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini yanayofanya kazi za kijamii ambazo awali usajili wake ulifanyika katika Mamlaka nyingine kama RITA, Msajili wa Jumuiya za Kijamii wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na BRELA usajili wake utakuwa umefutwa kama zitashindwa kujisajili chini ya Sheria ya NGO's kama iliyofanyiwa marekebisho na Sheria Na. 3 ya mwaka 2019 katika kipindi cha miezi miezi miwili toka tarehe 01 Julai, 2019.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dodoma Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Bi. Vickness Mayao ameyataka Mashirika hayo kutekeleza matakwa ya Sheria hiyo kwa mujibu wa Sheria na kuongeza kuwa zoezi linaloendelea la usajili Jijini Dodoma linalenga Mashirika hayo.

“Sheria inayataka Mashirika hayo kujisajili katika Sheria ya NGO's kwa kipindi cha miezi miwili hivyo huu ni wakati wa Mashirika kujitahimini yako wapi ili yaweze kufanya uamuzi sahihi kabla ya kipindi kilichotolewa na Sheria hii kupita.” Aliongeza Bi. Mayao.

Bi. Mayao amesema usajili huo kwa awamu hii unafanyika kwa mikoa ya Kanda ya Kati Tabora, Singida, Kigoma na Dodoma na kutoa wito kwa Mashirika yaliyopo katika Mikoa hiyo kufanya usajili huo akiongeza kuwa zoezi hili linafanyika bila malipo kwa Mashirika yanayouhisha usajili lakini Mashirika yanayojisajili mara ya kwanza yanatoa malipo kwa ajili ya huduma hiyo.

Bi. Mayao ameyataka Mashirika kusajili pia kwa njia ya mtandao kwani fomu za kujaza zinapatikana kwenye Website ya Msajili ambapo mtu anayetaka kusajili atajaza fomu hiyo lakini pia kuwasilisha Katiba dogo ikiwemo sifa za viongozi wa Shirika pamoja na eneo la utekelezaji au kusudio la shughuli za kazi za shirika.

Aidha Mwakilishi wa Msajili wa Jumuiya za Kijamii kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Bw.Thomas Sanila amesema kuwa Ofisi ya Msajili wa Jumuiya inashiriki usajili huo kuangalia kama kuna mkanganyiko wowote utakaojitokeza na kufuatilia kama shuguli zinazofanywa na Shirika husika zinaendana na Sheria na taratibu za Nchi.

Bi. Khadija Omari kutoka Taasisi ya Tuvuke Wote iliyoko Jijini Dodoma ameyataka Mashirika kujitokeza kwa wingi akisifu taratibu za usajili kuwa ni za haraka tofauti na alivyofikiria kwani ametumia takribani nusu saa kukamilisha zoezi la usajili.

Zoezi hili la usajili limeanza tangu tarehe 10 mwezi huu Jijini Dar es Salaam ambapo asilimia 80 ya NGO's zilizoko Kanda ya Mashiriki zimefanya usajili wake na zoezi la usajili linaendelea kwa kipindi cha miezi miwili kama ilivyo elekezwa katika marekebisho ya Sheria Na. 3 ya mwaka 2019. Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Bi. Vickness Mayao akizungumza na vyombo vya habari kuhusu usajili wa Mashirika ambayo hayakusajili kwa Sheria ya NGOs zoezi linaloendelea kwa Kanda ya Kati katika Chuo cha Mipango jijini Dodoma.
 Mwanasheria wa Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Bw. January Kitunsi (kushoto) akitoa huduma kwa wadau wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali waliofika katika Kituo cha Usajili wa Mashirika ambayo hayakusajili kwa Sheria ya NGO's zoezi linaloendelea kwa Kanda ya Kati katika Chuo cha Mipango jijini Dodoma.
Mwanasheria wa Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Bw. Denis Bashaka(kushoto)akitoa huduma kwa wadau wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali waliofika katika Kituo cha Usajili wa Mashirika ambayo hayakusajili kwa Sheria ya NGO's zoezi linaloendelea kwa Kanda ya Kati katika Chuo cha Mipango jijini Dodoma. Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...