Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Bw. Leonard Nkamba wa kijiji cha Kambanga wilayani Kasulu msaada wa sh. milioni 2.5 ili zimwezesha kununua vitendea kazi vya kisasa vya kumsadia kufanya kazi yake ya kuchonga vyombo mbalimbali vya mezani kwa kutumia miti. Makabidhiano hayo yalifanyika mjini Kigoma Julai 24, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

======  =======  ====== = =============

SERA YA VIWANDA YASAIDIA KUPUNGUZA TATIZO LA AJIRA

MKAZI wa kijiji cha Kabanga wilayani Kasulu mkoani Kigoma, Leonard Nkamba anayejishughulisha na uchongaji wa vyombo mbalimbali vya jikoni ameishukuru Serikali kwa kuanzisha sera ya viwanda kwa kuwa imesaidia kupunguza tatizo la ajira nchini.

Ameyasema hayo leo (Jumapili, Julai 14, 2019) baada ya kukabidhiwa kiasi cha sh. milioni 2.5 na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ili aweze kuongeza mashine itakayomuwezesha kuchonga bidhaa zenye ubora zaidi. Makabidhiano hayo yamefanyika mjini Kigoma.

Bidhaa anazochonga ni vikombe, chupa za chai, hot pot kwa kutumia mti aina ya jakalanda. Mbali na kutengeneza vyombo hivyo, pia mjasiriamali huyo ambaye ameajiri vijana watatu anachonga vibao na kuandika ujumbe mbalimbali kwa kutumia unga wa ngano.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa fedha hizo na Waziri Mkuu, mjasiliamali huyo amesema anaushukuru Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) ambao uliona kazi zake na kumuagiza atengeneze seti za vyombo kwa ajili ya zawadi za kumpelekea Rais Dkt. John Magufuli.

“Uongozi wa UWT mkoa wa Kigoma Taifa ulivutiwa na kazi zangu na kuniagiza nitengeneze chupa ya chai, vikombe na hot pot kwa ajili ya kumpa zawadi Mheshimiwa Rais pamoja na Waziri Mkuu ndipo Waziri Mkuu jana aliona kazi zangu na akavutiwa na bidhaa ninazotengeneza ndipo akaniuliza kama kuna changamoto zinazonikabili nikamwabia nahitaji mashine moja yenye thamani ya sh. milioni mbili na nusu akasema umepata na leo sijaamini alivyoniita na kunikabidhi. Namshukuru sana.”

Nkamata ametumia fursa hiyo kuwashauri wananchi wengine hususani vijana waache kulalamikia suala la ukosefu wa ajira na badala yake wajiunge katika vikundi vya ujasiriamali na kuzalisha bidhaa mbalimbali ambazo wataziuza na kujipatia kipato.

Pia amewaomba Watanzania wajenge utamaduni wa kutumia bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na viwanda vya ndani kwa kuwa vina ubora wa kutosha na pia watakuwa wanachangia kukuza uchumi wa wajasiriamali na Taifa kwa ujumla. Amesema bidhaa anazotengeneza ni rafiki wa mazingira kutokana na malighafi anazotumia.

Kwa upande wake Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwasihi wananchi kujishughulisha na shughuli mbalimbali za ujasiriamali ili waweze kujipatia kipato na kuondokana na umasikini. Pia amesema Serikali ipo tayari wakati wowote watakapohitaji msaada.

Waziri Mkuu amempongeza mjasiriamali huyo kwa bidhaa mbalimbali anazotengeneza ambazo ni nzuri na za kipekee. Amesemma amefurahi kuona vikombe, chupa za chai pamoja na hot pot zilizotengenezwa na Mtanzania kwa kutumia miti.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...