Zainab Nyamka, Michuzi Tv
Mkurugenzi wa ukaguzi  wa Ndani ( Internal Audit)  wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es salaam DAWASA Rosemary Lyamuya amesema wanahakikisha wakandarasi wanafanya kazi kulingana na makubaliano ya mkataba.

Rosemary ameyasema hayo alipotembelea banda la DAWASA lilipo kwenye maonesho ya 43 ya biashara ya kimataifa ndani ya Viwanja vya Mwalimu Nyerere Sabasaba barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam.

Amesema, kazi kubwa inayofanywa na kitengo chao ni kukagua miradi mbalimbali inayosimamiwa na Dawasa ambapo ni miradi ya maji safi na ile ya maji taka.

"Tunakagua miradi yote inayosimamiwa na Dawasa, ile maji safi na maji taka pamoja na kuhakikisha wakandarasi wanafanya kazi kulingana na makubaliano ya mikataba," amesema Rosemary.

Amesema, katika miradi inayokaguliwa na kitengo cha ukaguzi wa ndani (Internal Audit) wanahakikisha miradi inayojengwa na ile iliyomalizika kujengwa inaendana na mkataba pamoja na bajeti iliyopangwa.

Akizungumzia mikataba sita iliyosainiwa mapema wiki hii na Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Mhandisi Cyprian Luhemeja na wakandarasi mbalimbali, Kitengo cha ukaguzi wa ndani  wamejipanga  kusimamia na kukagua miradi yote  na kuhakikisha wakandarasi wanafanya kazi zao na kufuata mikataba inavyosema.

Mbali na hilo, Rosemary ameeleza kuwa inapotokea kuna kuhujumiwa kwenye miundo mbinu ya Dawasa wamekuwa wanatoa ushauri kwenye menejimenti ili wayafanyie kazi.

Ametoa rai kwa wananchi kutoa taarifa pale wanapoona kuna miundo mbinu ya Dawasa inahujumiwa, ikiwemo watu kujiunganishia maji kiholela kwani hilo linasababishia hasara kwa mamlaka na kushindwa kufikia malengo ya asilimia 95 mwaka 2020.
 Mkurugenzi wa ukaguzi  wa Ndani  ( Internal Audit) DAWASA Rosemary Lyamuya akizungumza na waandishi wa habari na kuwahakikishia wanachi miradi yote iliyosainiwa na DAWASA wanaikagua na kuisimamia ili iendane na makubaliano ya mkataba na inamalizika kwa muda uliopangwa. Hayo ameyasema wakati wa  maonesho ya 43 ya biashara ya kimataifa ndani ya Viwanja vya Mwalimu Nyerere Sabasaba barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa ukaguzi  wa Ndani (Internal Audit) DAWASA Rosemary Lyamuya akipata maelezo kutoka kwa Afisa ubora wa maji Sizya Mongela alipotembelea banda la Mamlaka hiyo wakati wa maonesho ya 43 ya biashara ya kimataifa ndani ya Viwanja vya Mwalimu Nyerere Sabasaba barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa ukaguzi  wa Ndani (Internal Audit) DAWASA Rosemary Lyamuya akipata maelezo ya vifaa vinavyotumia kuunganishia maji kutoka kwenye bomba na kupeleka kwa mteja ili apate huduma ya maji safi na salama wakati alipotembelea banda la DAWASA kwenye maonesho ya 43 ya biashara ya kimataifa ndani ya Viwanja vya Mwalimu Nyerere Sabasaba barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...