Na, Editha Edward-Tabora 

KIJANA Athuman Khamis ambaye ni Mkazi wa Kijiji cha Usongwa katika Kata ya Bukene wilayani Nzega mkoani Tabora anatuhumiwa kumuua kwa kumchinja bibi yake Rahel Daud(67)mkazi wa kijiji hicho huku Sababu ikielezwa ni uvutaji wa bangi kwa kijana huyo

Tukio hilo la kikatili limetokea jana saa 12 jioni katika kijiji cha Usongwa kata ya Bukene wilayani Nzega Mjini 

Mkuu wa Wilaya ya Nzega Godfrey Ngupulla amesema kwa upelelezi aliofanya hadi chanzo cha mauaji hayo ni kuwa uliotokea ugomvi mdogo wa kurushiana maneno kwa bibi huyo na kijana huyo na ndipo alipomvizia ndani na kumchinja kwa kumtenganisha kiwiliwili na shingo

Esther Salum ambaye ni ndugu wa Rahel Daud ameiambia Michuzi Blog kuwa kitendo hicho alichofanyiwa ndugu yake si kizuri, hivyo anaiomba Serikali kumtafuta kijana aliyefanya kitendo hicho ili afikishwe kwenye sheria.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya Nzega George Mgarega amesema kuwa mwili huo ulivyofikishwa hospitalini hapo ulifanyiwa uchunguzi na kuonekana ulikuwa na majeraha ya kukatwa na kitu chenye ncha kali kwa kuanzia nyuma na kwenda mbele hivyo kusababisha kuvuja kwa damu nyingi na maumivu makali na hivyo kupoteza maisha.

Wakati huo huo Jeshi la Polisi wilayani Nzega linaendelea kufanya uchunguzi wa kumtafuta kijana huyo aliyefanya mauaji hayo.
 Pichani ni Ndugu wa Marehemu Esther Salum akielezea kitendo hicho.
 Pichani ni Mwili wa Marehemu Rahel Daud aliyepoteza maisha kwa kuchinjwa na kijana Athuman Khamis Wilayani Nzega.
 Mganga  Mfawidhi Hospitali ya Wilaya  Nzega,George Mgarega  akielezea baada ya kufanyiwa uchunguzi Mwili wa Marehemu.
Mkuu wa Wilaya ya Nzega,Mh.Godfrey Ngupulla  akielezea jinsi tukio la Mauaji hayo  lilivyotokea.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...