Na.Khadija seif, Michuzi tv.

WAFANYABIASHARA wametakiwa kuona kama tunu na kuupa kipaumbele Mkutano
kwa nchi wanachama wa  Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), unaotarajiwa kufanyika nchini mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Auction Mart Alex Msama amesema Mkutano huo unatarajiwa kuhudhuriwa na zaidi ya watu 1,000 kutoka nchi mbalimbali.

"Mkutano huo wa 39 unatarajiwa kuhudhuriwa na wakuu wa nchi 16 wanachama wa jumuiya hiyo hivyo ni fursa pekee kufanyika ndani ya ardhi ya Tanzania na tutaweza kuongeza pato la taifa katika kila sekta hapa nchini,"

Aidha, Msama amesema mbali na kuongeza pato la taifa kupitia sekta mbalimbali bali pia tutaweza kupata fursa ya kufanya biashara mbalimbali ikiwemo mahoteli,vyakula pamoja na usafiri kutoka sehemu moja kwenda nyingine kupitia wageni watakaokuwepo nchini katika Mkutano huo.

"Ni wakati wa wafanyabiashara wenzangu kuzikimbilia fursa kwa kipindi hicho wageni watakapowasili kwenye Mkutano huo ambapo Rais wetu John Pombe Magufuli amekishika kijiti Cha kuendesha Mkutano huo akiwa kama Mwenyeji ,"

Pia Msama amesema kutokana na juhudi zinazoendelea kufanywa na serikali ya Mapinduzi chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hakuna ambae ataweza kumuangusha chini Rais huyo ifikapo 202o katika uchaguzi Mkuu.

"Katika kipindi chote alichokua Madarakani Rais Magufuli ameboresha kila sekta kuanzia elimu,usafiri,ajira, pamoja na Miundombinu mbalimbali na kwa wiki hii tunategemea kupokea umeme wa Rufiji ikiwa ni ishara tosha ya kuendelea kupokea wawekezaji kwa wingi bila kuwepo kwa kikwazo cha kukosa na kukatisha shughuli za uzalishaji viwandani kwa wawekezaji wetu,"
 Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promosheni na Msama Auction Mart, Alex Msama akizungumza na Waandishi wa habari mapema leo Ofisini kwake,jijini Dar kuhusu mambo mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujio wa mkutano mkubwa wa SADC.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...