Na Humphrey Shao, Michuzi Tv Dar es Salaam

Hospitali ya Taifa Muhimbili kupitia idara ya watoto imepokea Mashine mpya ya kisasa ya kuchunguza na kupiga picha kwa wagonjwa wa macho wanaofika hospitalini hapo.

Akizungumza na Waandishi wa habari Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Profesa Rawlence Mseru amesema mashine hiyo yenye uwezo wa kupiga picha nyuma ya retina itasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza tatizo la wagonjwa kutoka hospitalini happy kwenda kufanya vipimo sehemu nyingine.

"Mashine hii ya kisasa imenunuliwa na kikundi Cha kwaya ya watoto kutoka kanisa kuu London uingereza ambalo watoto hao walichangishana na kununua mashine hii yenye thamani zaidi ya milioni 100"

Kwa upande wake Dr John Kisimbi Daktari bingwa wa magonjwa ya macho kwa watoto katika Hospitali ya Taifa Muhimbili idara ya watoto Amesema kuwa kwa Sasa mashine hiyo katika hospitali hiyo ni Moja tu tangu ile iliyonunuliwa miaka ya nyuma kuharibika kutokana na kukaa kwa muda mrefu.

Ametaja kuwa uwepo wa mashine hiyo itasaidia kuhudumia wagonjwa wengi ambao walikuwa wanachelewa kupata huduma kutokana na vipimo vyao kuchelewa kutoka nje.
Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Profesa Rawlance Mseru akipokea kifaa hicho kutoka na kiongozi wa kundi la wasamaria wema kutoka nchini uingereza , Mathew Wright wakati wa hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika jengo la Watoto Muhimbili.

Afisa uhusiano wa Hospitali y Taifa Muhimbili,Aminiel aligaisha akizungumza na wafachili pamoja na wadau wa Hospitali ya Muhimbili.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...