Aliyekuwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu(TFF), Jamal Malinzi, Katibu wake Selestine Mwesigwa na wenzao wawili wamekutwa na kesi ya kujibu katika mashitaka 20 kati ya 30 yaliyokuwa yakiwakabili ikiwemo ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na utakatishaji fedha.

Wengine waliokutwa na kesi ya kujibu ni Mhasibu wa TFF, Nsiande Mwanga, na Karani Flora Rauya huku Meneja wa TFF, Mariam Zayumba akiachiwa huru.

Uamuzi huo umetolewa Julai 23,2019 na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Mhe. Maira Kasonde, k
esi hiyo ilipofika kwa ajili ya uamuzi mdogo kuona kama washtakiwa wana kesi ya kujibu ama la.

Akisoma uamuzi huo, Hakimu Kasonde amesema, upande wa mashtaka ulileta mashahidi 15 na vielelezo tisa katika kuthibisha kesi hiyo.

Amesema katika mashtaka 30 waliyokuwa wakikabiliwa nayo, yapo pia mashtaka ya matumizi mabaya ya madaraka dhidi ya Malinzi na Mwesigwa, shtaka la kula njama na kutoa nyaraka za uongo linalomkabili mshitakiwa Mwesigwa.

"Ni jukumu la mahakama kuangalia kama mshitakiwa ametajwa kwa namna yoyote katika mashitaka na ni upande wa mashitaka ambao wanatakiwa kuyathibitisha bila kuacha shaka yoyote mashtaka yote.

"Katika ushahidi wote uliotolewa mahakamani dhidi ya shtala la kula njama, hakuna chembe ya ushahidi kwamba mshitakiwa Malinzi na Mwesigwa walikula njama kufanya makosa ya kughushi hivyo.
"Ili kuthibitisha,  upande wa mashitaka ulitakiwa kuleta vielelezo vya kuonesha namna njama zilivyofanyika...Kwa mantiki hiyo mahakama inawaona washtakiwa hawana kesi ya kujibu kwenye shtaka hilo", alisema Hakimu Mkazi huyo.
Aliendelea kusema kwamba katika shtaka la matumizi mabaya ya madaraka, washtakiwa Malinzi na Mwesigwa wamekutwa na kesi ya kujibu kwani upande wa mashitaka walitengeneza kesi dhidi yao hivyo wanapaswa kujitetea.

Mshtakiwa Mwesigwa pia atatakiwa kujitetea katika shitaka la kutoa nyaraka ya uongo ya maazimio ya kamati tendaji ya Juni 5, 2016 kwa lengo la kuonesha kuwa kamati hiyo ya TFF imelenga kubadili mtia saini wa shirikisho hilo katika akaunti za benki kutoka Edgar Masoud kwenda kwa Mwanga.

Katika shtaka la tano hadi 14 la kughushi yanayomkabili Malinzi na Rauya, ushahidi ulionesha kuwa nyaraka iliyoghushiwa ambayo ni risiti ilitengenezwa na shahidi namba 10 ambaye ni Hellena Mihayo kwa kufuata maelekezo toka kwa Mkurugenzi wa Fedha.

Kwa upande wa mshitakiwa Rauya yeye anatakiwa kujitetea katika shitaka moja la kughushi risiti namba 00746 kwani ndiye aliyetengeneza nyaraka hiyo na hakuna ushiriki wa Malinzi katika mashitaka hayo.

Aidha, katika shitaka la saba mahakama imewaona washitakiwa kuwa hawana kesi ya kujibu kwani hakuna ushahidi unaowaunganisha na kesi hiyo.

Pia Hakimu Kasonde amesema katika kosa la kughushi la tisa, hati ya mashitaka inaonesha Malinzi na Rauya walighushi risiti namba 00870 ya Sh milioni 50 wakati kitabu cha risiti hiyo kinaonesha ni Sh milioni tano huku katika shtaka la 11, hati ya mashitaka inaonesha risiti 00947 iliyoghushiwa ni USD 10,000 lakini uhalisia ni USD 1000.

Ameongeza kuwa, mashitaka ya 15 hadi 26 ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu yanayomkabili Malinzi mahakama imemuona kuwa ana kesi ya kujibu na kumtaka kujitetea.

"Katika mashitaka ya 27 na 28 ya utakatishaji fedha yanamkabili Malinzi hivyo, atatakiwa kujitetea na katika mashitaka ya 29 na 30 ya utakatishaji fedha yanawakabili Mwesigwa na Mwanga mahakama inawaona na kesi ya kujibu hivyo mtatakiwa kujitetea," alisema Hakimu Kasonde.

Baada ya kusomewa hayo, mawakili wa utetezi wakiongozwa na Abrahamu Sembuji, Kashinde Thabiti wamedai wateja wao watajitetea chini ya kiapo na kuleta mashahidi.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Agosti 6, mwaka huu kwa ajili ya washtakiwa kuanza kujitetea.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Moja ya story zinazobamba mtaani ni kuifanya Kilimanjaro kuwa Nchi kabisa jambo la kujiuliza kwa muda wote huo ambao story hii imekuwa ikibamba kwenye vijiwe vya kahawa na ukichukulia nchi ya Tanzania ni kubwa kuliko BURUNDI, na RWANDA ni Mkoa GANI AMBAO HAUHITAJI KUWA NCHI?

    TANGA?

    MBEYA?

    RUVUMA?

    NJOMBE?

    N.K

    AU TUTUMIE REGRESSION ANALYSIS

    KUGAWA MIPAKA == a + b (mbunu za kupatia uongozi) + c(NI MKOA GANI HAUTAKI KUWA NCHI) + d (KWANINI USIWE NCHI) + e(TUPELEKE WAPI MAOMBI) + ERROT (hela) TERM (awamu ya urais/hela za msimu)

    KAMA KAWAIDA UKIWEKA MKOA WAKO (WEKA 1 WENGINE ZIRO (0)) MFANO IKIWA NACHIGWEA WEKA (1) ILI kwenye b upate NAMBA…

    BAADA YA HAPO INAKUWA time SERIES (MWAKA 1, 2, 3, 5, n.k)

    UJAMAA NA KUJITEGEMEA SONG

    https://www.youtube.com/watch?v=01zj7ulRK1s

    ReplyDelete
  2. Moja ya story zinazobamba mtaani ni kuifanya Kilimanjaro kuwa Nchi kabisa jambo la kujiuliza kwa muda wote huo ambao story hii imekuwa ikibamba kwenye vijiwe vya kahawa na ukichukulia nchi ya Tanzania ni kubwa kuliko BURUNDI, na RWANDA ni Mkoa GANI AMBAO HAUHITAJI KUWA NCHI?

    TANGA?

    MBEYA?

    RUVUMA?

    NJOMBE?

    N.K

    AU TUTUMIE REGRESSION ANALYSIS

    KUGAWA MIPAKA == a + b (mbunu za kupatia uongozi) + c(NI MKOA GANI HAUTAKI KUWA NCHI) + d (KWANINI USIWE NCHI) + e(TUPELEKE WAPI MAOMBI) + ERROT (hela) TERM (awamu ya urais/hela za msimu)

    KAMA KAWAIDA UKIWEKA MKOA WAKO (WEKA 1 WENGINE ZIRO (0)) MFANO IKIWA NACHIGWEA WEKA (1) ILI kwenye b upate NAMBA…

    BAADA YA HAPO INAKUWA time SERIES (MWAKA 1, 2, 3, 5, n.k)

    UJAMAA NA KUJITEGEMEA SONG

    https://www.youtube.com/watch?v=01zj7ulRK1s

    ReplyDelete
  3. VIONGOZI TUSIOWAFUATA (WAZEE)

    Moja ya story zinazobamba mtaani ni kuifanya Kilimanjaro kuwa Nchi kabisa jambo la kujiuliza kwa muda wote huo ambao story hii imekuwa ikibamba kwenye vijiwe vya kahawa na ukichukulia nchi ya Tanzania ni kubwa kuliko BURUNDI, na RWANDA ni Mkoa GANI AMBAO HAUHITAJI KUWA NCHI?

  4. VIONGOZI TUSIOWAFUATA (WAZEE)

  5. VIONGOZI TUSIOWAFUATA (WAZEE)

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...