Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

MBIO za Mwenge wa Uhuru kiaifa 2019 zinazoongozwa na Mzee Mkongea Ali zimetembelea Kisima cha Gezaulole kilichojengwa mwishoni mwa miaka ya sabini kinachokarabatiwa na Mamlaka ya Majisafi na Majitaka DAWASA.

Kisima cha Gezaulole kilisimama kufanya kazi mwaka 2010kutokana na kharibika mkwa pampu npamoja na ukarabati wa mabomba ambapo mwaka 2018 Manispaa ya Kigamboni iliomba uongozi wa DAWASA kufufua mradi huu ili utoe huduma ya maji kwa wananchi.

Mzee Mkongea amewataka wananchi kulinda vyanzo vya maji ili waweze kunufaika na miradi ya maji ya jamii ambapo katika Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitafa mwaka huu zimekusaidia kuoresha sekta ya maji pamoja na ushirikishwai wa wananchi kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa.

Amewaonya wakandarasi wanaojenga miradi chini ya kiwango na wengine kuchelewa kuimaliza kwa wakati na kuwa suala hilo halitafumbiwa macho na hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

Mkongea amesema, kuanzia mwaka 2006 hadi 2018 miradi 1659 imekamilika, na lengo la serikali kufikia 2020 wakazi wa vijijini asilimia 85 wanapata maji safi na salama na mijini kwa asilimia 95, ameongeza kwa kuanzia mwaka 2015 hadi 2018 miradi 124 imekamilika kwa upande wa mijini na na kuna miradi mingine mikubwa inaendelea kutekelezwa chini ya serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Dkt John Pombe Magufuli.

Kwa Mkoa wa Dar es Salaam, Mzee Mkongea ameweza kutembelea miradi mbalimbali ya DAWASA na wameridhishwa na utendaji kazi wa mamlaka hiyo inayoongozwa naMhandisi Cyprian Luhemeja.

Akisoma taarifa fupi, Msimamizi wa mradi huo kutoka DAWASA Mhandisi Lilian Masilago amesema kuwa kisima kilichopo Gezaulole kina uwezo wa kuzalisha Lita za ujazo 24,000 kwa saa na miundo mbinu mingine iliyopo ni pamoja na matanki mawili yenye ujazo wa Lia 90,000 na lita 60,000.

Lilian amesema, kisima hiki kipo chini ya Manispaa ya Kigamboni na kimegharimu zaidi ya Milion 154 zilizotumika kwa mfumo wa Force Account kutoka DAWASA na Milion 3 kutoka Halmashauri kwa ajili ya ufufuaji wa Bustani.

“Mradi wa Kisima cha Gezaulole unatarajia kuhudumia wananchi takribani 8000 katika maeneo ya Gezaulole, Mbwa maji na Kibugumo na kufufuliwa kwa mradi huu ni katika kumuenzi Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere ambaye ndiye aliyeanzisha huduma hii ya majia pamoja na bustani ya Gezaulole wakati wa uanzishwaji wa vijiji vya ujamaa,”amesema Lilian.

Aidha ameeleza changamoto mbalimbali katika mradi huo ikiwamo uvamizi wa eneo la tanki katika Mtaa wa Kizani ambapo tayari Halmashauri inalifanyia kazi.
 Msimamizi wa mradi huo kutoka Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam DAWASA Mhandisi Lilian  Masilago   akisoma taarifa  fupi ya mradi wa Kisima cha maji Gezaulole Kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa 2019 Mzee Mkongea Ali , kisima  hicho kitatoa huduma kwa wananchi 8000 baada ya kukamilika kwa ukarabati baaada ya kuharibika kwa pampu mwaka 2010.
  Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa uhuru Kitaifa 2019 Mzee Mkongea Ali akimtwisha mama ndoo kichwani baada ya kutembelea Tanki la maji lililopo eneo la Kizani linalopokea maji kutoka kwenye kisima cha Gezaulole.
 Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa uhuru Kitaifa 2019 Mzee Mkongea Ali akipanda mti kama kumbukumbu ya kumuenzi Baba wa Taifa Mwalimu Julius K Nyerere  katika Bustani ya Gezaulole wakati wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2019 ilipotembelea mradi wa Kisima cha maji cha Gezaulole.
  Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa uhuru Kitaifa 2019 Mzee Mkongea Ali akizungumza na wananchi wa eneo la Kizani lilipo tenki la maji  wakati wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2019 ilipotembelea mradi wa Kisima cha maji cha Gezaulole  
 Msimamizi wa Miradi ya Maji ya Jamii ww Mamlaka ya Majisafi na Majitaka DAWASA Charles Makoye akitoa maelezo ya Kisima cha Gezaulole kwa Kiongozi wa Mwenge Wa Uhuru Kitaifa 2019 Mzee Ali Mkongea baada kutembelea leo.

Kisima cha Maji cha urefu wa Mita 24 na pampu iliyofanyiwa ukarabati na Mamlaka ya Maji safi na Majitaka DAWASA.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...