Na Karama Kenyunko, Michuzi Tv

 Aliyekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) Wilaya ya Ilala, Norah Waziri maarufu kama Nora Mzeru amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni  akikabiliwa na tuhuma za kughushi cheti cha ndoa.

Wakili wa serikali , Benson Mwaitenda amedau leo Julai 12, 2019 mbele ya Hakimu Mkazi Anifa Mwingira kuwa Februari 4,1995 jijini Dar, es Salaam, mshtakiwa kwa nia ya kudanganya, alighushi cheti cha ndoa chenye usajili namba 00040078 kwa nia ya kuonesha kuwa alifunga ndoa na marehemu Silvanus Mzeru Februari 4, 1995 katika kanisa la Roman Catholic la Mburahati huku akijua kuwa si kweli.

Hata hivyo, mshtakiwa  amekana shtaka hilo na kudai kuwa marehemu huyo ni mume wake.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika na mshtakiwa yuko nje kwa dhamana baada ya kufanikisha kutimiza masharti yaliyowekwa na mahakama ambapo Mahakama imemtaka
mshtakiwa huyo kuwa na wadhamini wawili ambapo mmoja kati ya wadhamini hao atoke katika Taasisi inayotambulika kisheria.

Pia kila mdhamini alitakiwa kusaini bondi ya Sh milioni moja milioni. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Julai 17, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa ili kuangalia kama upelelezi utakuwa umekamilika ama la.

Awali, Oktoba 24,2018 mshtakiwa hiyo alifikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala na kusomewa shtaka la kughushi mbele ya hakimu mkazi Flora Hauled.

Hata hivyo, kesi hiyo ilifutwa mahakamani hapo kwa sababu mahakama ile haikuwa na mamlaka ya kusikiliza na kufunguliwa upya mahakamani hapo leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...