NAIBU Waziri wa  Mifugo na uvuvi Abdalah Ulega amegoma kuweka jiwe la msingi katika Zahanati ya Mwandege iliyopo Mkuranga mkoani Pwani kutokana na paa lililoezekwa kuwa chini ya kiwango.

Akizungumza na wananchi wa Mwandege wakati wa ziara yake katika jimbo la Mkuranga Ulega amesema kuwa jengo hilo tayari linahitilafu kwasababu bati zote zinakutu.

"Kwa kweli mtanisamehe sitaweka jiwe la msingi, wenyewe mmekiri hapa katika risala yenu mapungufu ya paa hapa nawaagiza rekebisheni mapungufu yaliyojitokeza ili wananchi hawa wapate haki yao ya huduma,"amesema Ulega.

Aidha Ulega amesema atamuagiza Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Filibeto Sanga na timu yake yote ya kamati ya ulinzi na usalama kufika eneo la Zahaati ili kufanyia uchunguzi kufahamu nani au kitu gani kilijitokeza mpaka kufikia bati kuwa na kutu.

Ulega amesema ili kulinda haki ya wananchi wa Mwandege ni lazima jambo hilo lichunguzwe na wale wote waliofanya ubabaishaji na kubainika wamehujumu ujenzi huo,hatua kali zichukuiwe dhidi yao sambamba na kulipa bati hizo.

Hata hivyo amesisitiza  uchunguzi ukibaini kwamba kumetokea kasoro ya bahati mbaya basi wa mwandikie barua,na yeye atakuwa tayari kugharamia bati zote 250 zinazohitajika kwa ajili ya ukarabati na ikitokea vinginevyo wahusika watalipa.

"Ninavyojua jengo kila linavyo fika hatua moja ya ujenzi lazima likaguliwe,sasa sijui ilikuwaje jengo hili likaezekwa,lazima wataalamu watuambie haliyehusika na hao majina walifanyaje mpaka ikafika hivi,"amesema

Sambamba na hilo Ulega pia amebainisha  mpaka sasa Serikali  imeshachangia kiasi cha Sh milioni 30 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa zahanati hiyo.

Kwa upande wake Diwani wa kata ya Mwandege Adolf Kohelo amesema mhandisi kutoka halmashauri alishakuja na kueleza kuwa hitilafu hiyo sio ya bahati mbaya bali ni la makusudi yaliyofanywa na wahusika kwa aslahi yao binafsi.

Adha Kohelo amessema mtaalamu huyo pia alishauri kubadilishwa kwa mbao zilizotumika kuezekea paa hilo kwani haziimili uzito wa kwakuwa nyembamba.

Hata hivyo amesema mpaka sasa zaidi ya milioni kumi na nne zinahitajika ili kuweza kuezeka jengo hilo.
 Muonekano wa Mabati ya Zahanati hiyo aliyogoma kuweka  jiwe la msingi kwa kutoridhishwa na ujenzi.
 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Mbunge wa Mkuranga,Abdallah Ulega  akikabidhi mifuko ya Saruji 50 kwa viongozi wa  kata ya Mwandege kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa shule ya msingi  Lugwadu jana.Picha na (Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)
 Mkutano ukiendelea.
 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Mbunge wa Mkuranga,Abdallah Ulega  akiweka Howe la msingi katika shule ya ya msingi Lugwadu ambapo alikabidhi mifuko 50 ya Saruji kwa ajili ya shule ya msingi  Lugwadu jana.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Mbunge wa Mkuranga,Abdallah Ulega akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mwandege ambapo aligoma kuweka jiwe la msingi katika zahanati hiyo  kwa kutoridhishwa na ujenzi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...