Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi,Mkuu wa Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa ambaye pia ni mlezi wa Mkoa wa Geita,Ndugu Ngemela Lubinga ameanza ziara ya kikazi Mkoani Geita na amewasili wilaya ya Bukombe na kupokelewa na viongozi wote wa Mkoa wa Geita wa Chama na Serikali pamoja na Mbunge wa jimbo hilo Ndg.Dotto Biteko. 

Lengo la ziara hiyo ni kuhamasisha uingizaji wa wanachama kwa njia ya kielekroniki na kubaini changamoto za uingizaji wa wanachama kwa njia ya mfumo huo,pamoja na kukagua uhai wa chama na Jumuiya zake na atafika katika kila wilaya pamoja na kata na kuzungumza na viongozi wa ngazi ya matawi na mashina pamoja na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi. 
Wakati huo huo alipata nafasi ya kuzungumza na kamati ya Siasa ya Wilaya ambapo alipokea taarifa fupi ya kazi ya Chama Cha Mapinduzi na Jumuiya zake pamoja na hilo akawaambia “ninyi viongozi wa wilaya mnalo jukumu kubwa la kuhakikisha viongozi wa kata,shina na matawi wanashikamana na kuwa wamoja na kuwaheshimu tunaowaongoza”. 

Ndugu Ngemela Lubinga amewaambia viongozi hao kuwa dhamana waliyonayo ni kubwa hivyo waitumie vyema kuhakikisha wanakwenda kwa wananchi kuwaelezea mambo yote makubwa yaliyofanywa na Mheshimiwa Rais Dkt.John Pombe Magufuli ili wajue kazi kubwa inayofanywa na Serikali ya CCM maana Watanzania wengi ni waungwana sana. 

Naye Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa Mkoa wa Geita Ndugu.Iddi Kassim Iddi alipata nafasi ya kukabidhi ahadi yake ya jezi kwa timu nne za mpira alizokuwa ameahidi vijana wa Bukombe mbele ya mlezi huyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...