Na Woinde Shizza Michuzi Tv,Arusha

RAIA 19 wa Nchi ya Burundi wamefungua kesi katika mahakama ya Afrika mashariki dhidi ya serikali yao kupinga vitendo vya unyanyasaji wa haki za binadamu unaoendelea Nchini humo.

Wakizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha Mara baada ya kusajiriwa kwa kesi yao, baadhi ya mawakili kutoka chama cha wanasheria Afrika (PALU) wanaosimamia kesi hiyo,Evelyn Chijorira kutoka nchini Zimbabwe, alisema kuwa, wananchi hao kutoka Taifa la Burundi wamefungua shauri la haki ya Ardhi lenye namba 16/2019 katika mahakama hiyo.

Wakili huyo alisema kuwa, mwaka jana serikali ya Burundi iliwashtaki mahakamani wananchi wake wapatao 32 waliokuwa wakipinga Rais wa Burundi kushika madaraka kwa awamu ya tatu , lakini cha kushangaza kabla ya kesi hiyo kumalizika walisikia Ardhi yao,Nyumba zimetaifishwa na serikali ya Burundi.

"Tumekuja hapa katika mahakama ya Afrika mashariki kuwakilisha wananchi 19 wa Burundi kufungua kesi dhidi ya serikali yao wakilalamikia manyanyaso na kupokonywa Ardhi na Nyumba zao na serikali ya Burundi" Alisema

Aliongeza kuwa, mwaka jana kulitokea vurugu kwa wananchi kupinga rais wa nchi hiyo kujiongezea muda wa madaraka kwa awamu ya tatu jambo lililopelekea baashi yao kukamatwa na wengine kuikimbia nchi yao na kukimbilia mafichoni katika nchi mbalimbali.

Hata hivyo wakiwa nchi za Ng'ambo walisikia Ardhi zao na Nyumba vimechukuliwa na serikali ya Burundi jambo ambalo limewalazimu kufungua kesi katika mahakama ya Afrika Mashariki kudai haki zao na kupinga manyanyaso yanayotokea dhidi ya raia na nchi ya Burundi ikiweni kunyimwa Uhuru wa kujieleza, hali ambayo imechangia baadhi yao kuikimbia nchi yao.

"Ktokana na unyanyasaji huo kati ya wananchi hao 32 wananchi 19 wamekuja kufungua kesi katika mahakama hii ili kudai haki zao za kunyanganywa ardhi, nyumba na kutopewa Uhuru wa kujieleza. "alisema Wakili huyo.

Naye Wakili mwingine,anayewatetea walalamikaji hao Gustave Niyonzima kutoka Burundi alisema kuwa, yeye na mawakili wenzake wanne ambao wanawatetea wananchi hao 19 wa Burundi wamefungua kesi hiyo wakiwa na matumaini ya kupata haki kwa wananchi hao.

Alisema kuwa, wanaiomba mahakama hiyo iweze kusaidia watu wa Burundi wapate haki zao kutokana na kunyanganywa ardhi yao, nyumba na hata kunyimwa Uhuru wa kuzungumza wakati hiyo ni haki ya kila mmoja.

"Tunamatumaini makubwa na hii mahakama kuwa haki itatendeka ili raia wa Burundi waweze kupata amani na uhuru na hatimaye kuweza kumiliki mali zao. "alisema Wakili Niyonzima.

Kwa mujibu wa Mawakili hao kesi hiyo itapangiwa siku rasimi ya kuanza kusikilizwa baada ya upande wa serikali ya Burundi kujulishwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...