Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli anatarajiwa kuwa mageni rasmi katika ufunguzi wa maonensho ya wiki ya Viwanda kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) yatakayofanyika Jijini Dar es Salaam kuanzia Agosti 5, 2019 

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini humo Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Innocent Bashungwa amewaasa Watanzania kujitokeza kwa wingi na kutumia fursa ya maonesho ya wiki hiyo yatakaofanyika kwa lengo la kuhamasisha na kukuza ujenzi wa uchumi wa viwanda na kukuza masoko kwa nchi wanachama. 

“ Tayari washiriki 580 wameshajiandikisha kushiriki maonesho hayo na matarajio yakiwa washirki zaidi ya 1000 kutoka katika nchi wanachama wa SADC na tunachoangalia kwa sasa ni namna maonesho ya wiki ya viwanda yatakavyowanufaisha Watanzania kwani hii ni fursa ya wazalishaji wetu na wamiliki wa viwanda kutangaza bidhaa zao na kupanua wigo wa masoko katika nchi wanachama “ Alisisitiza Mhe Bashungwa 

Akifafanua Mhe Bashungwa amesema kuwa amani na mshikamano uliopo hapa nchini ni msingi wa maendeleo ya sekta ya viwanda na sekta mbalimbali hapa nchini hali inachangia kukuza ustawi wa wananchi na kujenga uchumi jumuishi. 

Faida za maonesho hayo ni pamoja na kukuza masoko, kuongeza na kupanua wigo wa uwekezaji katika sekta ya viwanda na pia kuwaleta pamoja wafanyabiashara wa nchi wanachama kupitia jukwaa la biashara litakalozinduliwa wakati wa wiki ya Viwanda. 

Aidha, Mhe Bashungwa amesema kuwa Tanzania kuwa mwanachama SADC na katika Jumuiya mbalimbali ni fursa ya wananchi kuongeza uzalishaji wenye tija unaolenga kukuza sekta ya Viwanda. 

Wiki ya viwanda itahitimishwa kwa washiriki kutembelea maeneo ya Viwanda jijini Dar es Salaam, ikiwemo eneo la ukanda maalum wa uwekezaji na kujionea utekelezaji wa shughuli za uzalishaji zinavyoendeshwa. 

Wiki ya Viwanda kwa nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika itafanyika kuanzia Julai 5 hadi 8 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya shughuli za kuelekea mkutano wa wakuu wa nchi na Serikali wa SADC utakaofanyika Agosti 17 na 18 Jijini humo. 
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Innocent Bashungwa akielezea faida za
maonesho ya wiki ya viwanda kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo yaKusini mwa Afrika (SADC) yatakayofanyika Jijini Dar es Salaam katika ukumbi waKimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere kuanzia Julai 5 hadi 8, 2019 ikiwa nisehemu ya matukio yatakaofanyika kuelekea mkutano wa wakuu wa nchi na Serikali wa SADC.
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Innocent Bashungwa akisisitiza kuhusu
hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kuhakikisha ujenzi wa uchumi wa viwanda unaleta matokeo chanya hapa nchini na katika mataifa wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...