Na.Vero Ignatus,Arusha.

Maadhimisho ya sherehe za kutimiza miaka 80 ya Kanisa la TAG pamoja na hitimisho la miaka 10 ya mavuno yaataandhimishwa wiki hii Jijini Arusha .

Dkt.Barbanas Mtokambali, Askofu Mkuu wa Kanisa la TAG nchini,  amesema katika mkutano wake na waandishi wa habari kuwa kanisa hilo likianza kazi nchini mwaka 1939, Igale mbeya ambapo hivi sasa yapo makanisa 9,986, vyuo vya Biblia 8 vyuo vya kupanda makanisa ,shule za sekondari,vyuo vya ualimu ambavyo vinakaribia kukamilika,vituo vya Radio,vyuo vya ualimu,vituo vya Afya na vituo vya huduma za jamii kwa watoto yatima.

Dkt.Mtokambali anasema mpango mkakati wa awamu ya kwanza ya mafanikio ya kanisa wameyapata katika miaka 10 ya mavuno kwani majimbo yameongezeka kutoka 10-69,makanisa 2,619-9,986,wachungaji 2,616-10,085,washirika kuongezeka 200,069-13,326,vyuo vya Biblia 4-8 ambapo Idara ya kujenga shule za sekondari na nyingine zitaanza kuandikisha wanafunzi mwezi Januari 2020.

Maadhimisho hayo yanaambatana uwekaji wa Jiwe la msingi wa Kanisa la kwanza la TAG kanda ya kaskazini Calvary Temple,Uzinduzi wa visima viwili maeneo ya Ngaramtoni,Makuyuni mmkoani hapa,Upimaji wa na Matibabu ya macho itakayofanyika kwa mMrmombo na Levolosi mkoani hapa 

Askofu huyo amesema hadi sasa kanisa hilo limeweza kutoa vitendea kazi mbalimbali kwa Maaskofu na waangalizi wa majimbo,pamoja na makatibu wa Kanisa hilo la TAG.“Kanisa letu hivi sasa linaonekana katika kila wilaya na kila kata ya Tanzanzania” Alisema Dkt.Mtokambali.

Ameeleza mwezi April 2019 wamekuwa na mfululizo wa sherehe za maadhimisho kuanzia kanisa la mahali pamoja,Jimbo,Idara na vyuo vya Biblia wakiwa na kauli mbiu isemayo “Ebenezer,hata sasa Bwana ametusaidia.”

Kwa upande wake Muhubiri huyo wa Kimataifa Johannes Amritzer amesema wao wanafanya ya uhubiri wa Injili inayogusa kila nyanja ya Jamii,kwani kuimba nyimbo.za kidini na kusoma maandiko hayabadilishi maisha ya mtu hadi mtu apate badiliko la ndani ya moyo.

Amesema yeye alilelewa maisha ya mtaani bila kuwa na uangalizi wa kutosha kutoka kwa wazazi kwani alikuwa mtukutu hadi pale Mungu alipoamua kuyabadilisha maisha yake na kuwa mtu mwingine na kuanza hatua mpya ya mabadiliko.

Amesema wiki hii ya kilele cha maadhimisho hayo kutakuwa na matukio mbalimbali kama Mkutano mkuu wa Halmashauri siku ya kesho,Baraza la waangalizi wote ,Mkutano wa wachungaji utafanyika chuo cha Ufundi Arusha pamoja na mkutano mkubwa wa Injili utakaoongozwa na Muhubiri wa Kimataifa Johanes Amritzer utakaofanyika uwanja wa Stadium wa Shekh Amri Abeid.

Aidha amesema julai 21 ndiyo itakuwa kilele cha maadhimisho ya sherehe hizo ambapo mgeni Rasmi anatazamiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli. 
Ambapo kwa pamoja wanasema “Miaka 10 ya mavuno -Kazi tuliyoianzisha.
Ikumbukwe kuwa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) lilianzaishwa mnamo mwaka 1939 Igale Mkoani Mbeya ambapo mwaka 2019 linatimiza miaka 80.
Askofu Mkuu wa Kanisa la TAG Dkt.Barnabas Mtokambali akizungumza na waandishi wa habari leo katika ukumbi uliopo hoteli ya Cordo Spring Jijini Arusha.
Mhubiri wa Kimataifa Johannes Amritzer
akizungumza na waandishi wa habari leo katika ukumbi uliopo hoteli ya Cordo Spring Jijini Arusha.
Mwenyekiti wa Maandalizi ya Sherehe hizo na Askofu wa TAG Mkoani Arusha O.Sosi akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusiana na ratiba ya shughuli nzima itakavyokuwa katika Sherehe hizo za miaka 80 ya kanisa la.TAG Tanzania.
Waimbaji wa Muziki wa Injili watakaohudumu katika Mkutano kutoka kushoto ni Julia Wilkander akiwa na Muimbaji Miriam Mauki kutoka nchini Tanzania
Askofu Mkuu wa Kanisa la TAG Dkt.Barnabas Mtokambali akiteta jambo na Mhubiri wa Kimataifa Johannes Amritzer.
Baadhi ya Timu itakayoshiriki katika sherehe hizo pamoja na mkutano mkuu wa Injili utakaoanza tar 17julai 2019 wakiwa tayari katika maandalizi.
Baadhi ya Timu itakayoshiriki katika sherehe hizo pamoja na mkutano mkuu wa Injili utakaoanza tar 17julai 2019 wakiwa tayari katika maandalizi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...