Mkuu wa Iringa Alli Hapi akitoa akiwahutubia wakazi wa Miyomboni mjini Iringa wakati wa ziara yake ya kuhamasisha ufunguzi wa stendi mpya ya mkoa eneo la Igumbilo nje kidogo na mji wa Iringa iliyoanza kutumika jana 
Mwenyekiti wa kamati ya usalama barabarani mkoa wa Iringa Salim Abri Asas (kulia) akimkabidhi fedha kiasi cha shilingi 500,000 kijana Maniani Mwakajenge ambae ni mjasiriamali aliyevunjwa mguu wake na polisi baada ya kijana huyo kulalamika katika mkutano wa hadhara wa mkuu wa mkoa wa Iringa Alli Hapi juu ya polisi kushindwa kumlipa gharama za matibabu kiasi cha Shilingi milioni 1 pamoja na Asas kumsaidia pia mkuu wa mkoa alimchangia Tsh 500,000 kijana huyo 
(Picha na Francis Godwin) 


…………………….. 
NA FRANCIS GODWIN, IRINGA 
Mkoa wa Iringa Alli Hapi ameliagiza jeshi la polisi kuwakata mshahara kiasi cha shilingi milioni 1 askari wake 10 waliohusika kumvunja mguu kijana Maiman Mwakajenge akiwa katika shughuli zake za ujasirimali . 
Kuwa fedha hizo watakazokatwa apewe kijana huyo aliyevunjwa mguu kama sehemu ya kulipia gharama zake za matibabu alizotumia baada ya kuvunjwa mguu na askari hao . 

Mkuu huyo wa mkoa alitoa agizo hilo kwa kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Juma Bwire jana jana katika eneo la stendi kuu ya mkoa baada ya kijana huyo Mwakajengela kulalamika kwenye mkutano wa mkoa huyo wa mkoa kuhusu kutotendewa haki na jeshi la polisi baada ya kuvunjwa mguu. 
Kijana huyo alimweleza mkuu wa mkoa kuwa Februari 2 mwaka huu akiwa katika shughuli zake za biashara eneo la Samora mjini Iringa alikutana na askari polisi waliokuwa doria ambao walimchukua na kumpakia katika gari la polisi na kuanza kumshambulia kwa kipigo na kumvunja mguu wake wa kushoto . 

“ Askari hao walichukua uamuzi wa kunipiga hadi kunivunja mguu wakidai kuwa nimewatukana na baada ya kunivunja mguu nilifanyiwa upasuaji Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa kwa gharama zangu kabla ya uongozi wa chama cha machinga mkoa wa Iringa kuingilia kati na kukaa na jeshi la polisi ambao waliahidi kuwa watakuwa akitoa fedha ya chakula na matibabu kwa ajili yangu na familia ila hadi leo hawafanyi hivi na nawadai kiasi cha shilingi milioni 1 hadi sasa naomba mheshimiwa mkuu wa mkoa nisaidie maana hadi hivi sasa ninatembea na chuma mguuni “ alisema kijana huyo. 

Kwa upande wake Hapi alimtaka kamanda wa polisi mkoa wa Iringa kwa kuwa anataarifa ya kuwepo kwa tukio hilo lililofanywa na askari wake kuwafuata askari wote waliohusika ambao hata hivyo wanafahamika na kuwakata fedha zao za mshahara ili kumlipa kijana huyo fedha yake anayowadai ya gharama za matibabu na chakula kwa muda wote ambao alikuwa Hospitali kiasi hicho cha Tsh milioni 1 anayowadai. 

‘’ Ninakuagiza RPC Bwire fyeka misharaha yao askari sio una posho zao za mishahara Nikishuka kama mwewe nikawadokoa itakuwa balaha sawa bwana utapewa shilingi milioni 1 na mimi kama mkuu wako wa mkoa nitakuchangia shilingi 500,000 na MNEC Salim Asas nae namsemea atakuchangia shilingi 500,000” alisema mkuu huyo wa mkoa huku akimkabidhi fedha taslim kutoka kwake na MNEC Iringa kiasi cha shilingi milioni 1 

Hata hivyo kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Juma Bwire alithibitisha kuwepo kwa tukio hilo na kuwa atalifanyia kazi kwa wakati . 
Katika hatua nyingine mkuu huyo wa mkoa ametangaza kuvifuta viwanja vyote vilivyopo mbele ya stendi kuu ya mkoa wa Iringa iliyojengwa eneo la Igumbilo viwanja ambavyo walijimilikisha watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa na baadhi ya madiwani kuwa viwanja hivyo vitatumika kwa ajili ya wananchi kujenga maduka ya biashara kuzunguka stendi hiyo . 

“ Haiwezekani stendi kubwa kama hii iliyojengwa na serikali kwa shilingi bilioni 3 kujengwa bila maduka ya biashara ama kutenga maeneo ya wafanyabiashara kufanyia shughuli zao ila nimebaini kuwa viwanja vyote vya mbele wamejigawia wao ili kuja kunufaika wao na stendi hii sasa sitaangalia kiwanja kinamilikiwa na naibu meya ama Meya , diwani ama mtumishi wa Manispaa kuanzia sasa nimevifuta vyote na sitaki suala hili kujadiliwa kwenye baraza la madiwani nataka wananchi wote wapate maeneo ya biashara sio vkiongozi “ alisema Hapi .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...