Na Humphrey Shao,Michuzi Tv Dar es Salaam

Mchezaji wa soka wa kimataifa na kulipwa anayekipiga na klabu ya Genk ya nchini Ubelgiji na nahodha wa kikosi Cha Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars Mbwana Sammata amesaini mkataba wa kuwa balozi wa Utalii kutangaza vivutio vya Tanzania nje ya Nchi.

Akizungumza na Waandishi was Habari mapema leo jijini Dar es Salaam katika hafla ya kusaini mkataba huo Samatta Amesema kuwa mkataba huo wa kujitolea utaanza Leo na utadumu kwa kipindi Cha miaka miwili.

"Mkataba huu nimesaini leo sio wa malipo kwani Mimi Kama kijana mzalendo nitaendelea kuitangaza Tanzania nje ya Nchi rasmi Kama balozi mteule wa bodi ya Utalii hivyo kazi hii naifanya kwa moyo wangu wote bila ya kupata malipo yoyote kutoka bodi hivyo ileweke hivyo"Amesema Samatta.

Akizungumza kwa niaba ya bodi ya Utalii Tanzania Mkurugenzi wa bodi hiyo Devota Mdachi Amesema kuwa makubaliano waliyotiliana saini leo ni ya kumfanya Samatta kuwa balozi wa hiari wa Utalii wa Tanzania popote pale atakapokuwa Duniani.

"Heshima ya ubalozi wa Utalii wa Tanzania tunaitoa kwa watu mbalimbali watanzania na hata wasio watanzania ili mradi tu ni watu waliokidhi vigezo na ambao tunaamini wanamapenzi na uzalendo kwa Nchi yao na wanaweza kweli kutusaidia kuvitangaza vivutio vyetu na utalii wetu wa Tanzania" Amesema Mdachi.

Amesema kwa mujibu wa mkataba huo bodi ya Utalii pamoja na mambo mengine TTB itakuwa ikimuandalia Samatta ziara za kutembelea maeneo mbalimbali ya vivutio vya Utalii angalau Mara Mona kila mwaka.

Ametaja ziara hiyo Samatta ataruhusiwa kuambatana na watu wasiozidi watano wakiwemo Waandishi was Habari ambapo gharama za usafiri wa ndani,malazi na chakula vutabebwa na TTB hivyo Samatta atachagua muda atakaikuwa na nafasi ya kufanya ziara hiyo.

Amesema pia TTB itatumia picha za Mbwana Samtta kwa ajili ya matangazo mbalimbali ya kuhamasisha Utalii iwe kwa njia ya televisheni ,radio ,mabango ya matangazo na kadhalika.
 Nahodha wa Timu ya Taifa ya Tanzania na Mshambuliaji wa Genk ya Ubelgiji, Mbwana Samatta akibadilishana mkataba na Mkurugenzi wa bodi ya Utalii Tanzania, Devota Mdachi
 Mwenyekiti wa bodi ya Utalii Tanzania Jaji Thomasi Mihayo akijadili Jambo na Mbwana Samatta na Mkurugenzi wa bodi ya Utalii Tanzania Devota Mdachi Mara baada ya mkutano wao na wanahabari
Mkurugenzi wa bodi ya Utalii Tanzania,Devota Mdachi akifafanua Jambo kwa Waandishi wa Habari leo juu ya ziara ya China na Korea ya kusini.

 Mwenyekiti wa bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Jaji      Thomas Mihayo akizungumza na Waandishi wa juu ya tathmini ya ziara ya China na Korea.
 Jaji Thomasi Mihayo akizungumza na Waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam.
 Nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania na Mshambuliaji wa Klabu ya Genk ya nchini Ubelgiji, Mbwana Samatta akizungumza na Waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam kabla ya kusaini mkataba wa kuwa balozi wa kutangaza vivutio vilivyopo Nchini.

 Mkurugenzi wa bodi ya Utalii Tanzania,Devota Mdachi pamoja na Nahodha wa Timu ya Taifa na Mshambuliaji wa Klabu ya Genk, Mbwana Samatta wakisaini makubaliano ya Samatta kuwa balozi wa Utalii nje ya Tanzania.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...