Na Zainab Nyamka, Michuzi Tv
Shirika la Save the Children limesherehekea kutimiza kwa miaka 100 toka kuanzishwa kwake sambamba na kuzindua mkakati wa miaka mitatu wa kuwalinda na kuwajali watoto.

Mkakati huo unaoanzia mwaka 2019 hadi 2021 kwa ajili ya watoto Tanzania umewekwa kwenye vipengele saba ambazo zitaangaliwa changamoto zinazowakabili watoto nchini.

Akizungumzia mradi huo, Kaimu Mkurugenzi Idara ya Watoto Wizara ya Afya, Jinsia, Wazee na Watoto Idara kuu ya maendeleo ya Jamii Mwajuma Magwiza amesema shirika la save the Children ni wadau wakubwa na wamekuwa wanashirikiana na serikali katika kusaidia na kuwalinda watoto.

Magwiza amesema, shirika hilo lipo nchini kwa miaka 30 na wanafanya kazi kulingana na mipango ya serikali kwa kuangalia namna gani wanawalinda watoto na wamekuwa wakiandaa mikakati mizuri inayomlinda mtoto.

Amesema, wamekuwa wanasaidia kutoa elimu rika kwa vijana waliobalehe, kuwawezesha watoto kielimu na kujitambua jambo ambalo limekuwa na msaada mkubwa sana kwa taifa.


Kwa upande wa Save the Children, mpango mkakati wao uliweza kutambulishwa rasmi unaoelezea mambo saba watakayoyaangalia ndani ya miaka mitatu.


Tuma Nkwabi, ameeleza kuwa malengo yao nchini Tanzania ni kuwalenga watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu zaidi. Malengo hayo ni Ishi ambapo mtoto atahitaji afya na lishe, Jifunze ikilenga elimu, Lindwa ikiwa ni Ulinzi wa mtoto, Umasikini wa mtoto na usimamizi wa haki za mtoto.

Malengo yao ni kushirikiana na mashirika yenye mtazamo mmoja ili kuwanufaisha watoto.

Mkurugenzi wa Save the Children nchini Peter Walsh amesema wamejikita zaidi katika kuangalia ni namna gani wanamsaidia mtoto na hata katika kutimiza miaka 100 ya shirika hilo waliweza kumleta Anne Chamberlain aliyeigiza na kuelezea stori ya Eglantyne Jebb aliyeweza kujitoa na kuwasaidia watoto waliokuwa wanaishi mazingira magumu nchini Ujerumani  na ndiye mwanzilishi wa Save the Children.

Sherehe hiyo ilihidhuriwa na watu mbalimbali na ilihitimishwa kwa wageni kutazama igizo kutoka kwa Anne Chamberlain.
 Kaimu Mkurugenzi Idara ya Watoto Wizara ya Afya, Jinsia, Wazee na Watoto Idara kuu ya maendeleo ya Jamii Mwajuma Magwiza  akikata keki pamoja na Mkuruge zj wa Save the Children Nchini Tanzania Peter Walsh wakati wa kusherehekea miaka 100 toka kuanzishwa kwake pamoja na kuzindua mkakati wa miaka mitatu utakaoanzia 2019 hadi 2022 wa kuwalinda na kuwajali watoto.
 Kaimu Mkurugenzi Idara ya Watoto Wizara ya Afya, Jinsia, Wazee na Watoto Idara kuu ya maendeleo ya Jamii Mwajuma Magwiza  akifuatilia kwa makini maelezo kutoka Save the Children kuhusiana na mkakati wa miaka mitatu utakaoanzia 2019 hadi 2021 wa kuwalinda na kuwajali watoto. 

 Wageni waalikwa mbalimbali wakifuatikia uzinduzi wa mkakati wa miaka mitatu wa kuwalinda na kuwajali watoto sambamba na sherehe ya miaka 100 ya Save the Children toka kuanzishwa kwake.
 Wageni waalikwa mbalimbali wakifuatikia uzinduzi wa mkakati wa miaka mitatu wa kuwalinda na kuwajali watoto sambamba na sherehe ya miaka 100 ya Save the Children toka kuanzishwa kwake.
 Mwakilishi kutoka Save the Children Touma Nkwabi  akielezea mkakati wa miaka mitatu utakaoanzia 2019 hadi 2021 wa kuwalinda na kuwajali watoto uliozinduliwa na Shirika lao.

 Wageni waalikwa mbalimbali wakifuatikia uzinduzi wa mkakati wa miaka mitatu wa kuwalinda na kuwajali watoto sambamba na sherehe ya miaka 100 ya Save the Children toka kuanzishwa kwake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...