Na Chalila Kibuda, Michuzi TV

Serikali imetengeneza miradi mbalimbali katika kuhakikisha jamii inapata huduma bora.

Hayo aliyasema Askofu Mkuu wa Kanisa la Calvary Assemblies of God (C.A.G) Ubungo Dunstan Maboya wakati wa Jubilee ya Miaka 25 ya Kanisa hilo.

Askofu Maboya amesema kuwa serikali inakwenda katika kuandaa mkutano wa Nchi zilizopo Kusini Mwa Afrika (SADC) ambapo Tanzania itanufaika na mkutano huo katika katika adhima ya kwenda uchumi wa Kati wenye Viwanda.

Amesema kuwa nchi imepiga hatua katika Ujenzi wa Barabara, Reli za Kisasa pamoja na ununuzi wa ndege ambapo inafanya watanzania kutembea kifua mbele.

Aidha amesema kuwa wananchi kama watu wa imani wanajifunia huduma zinazotolewa na serikali ikiwa na pamoja na wao kujenga huduma za jamii zikiwemo Hospitali pamoja na Shule.

Askofu amesema wakati wanaanzisha Kanisa hilo watu walijitoa kwa fedha zao kuhakikisha neno la Mungu linasimama .Askofu Maboya amesema kumtumikia Mungu sio lelema ni lazima uwe na imani kwani wengine walipoanzisha Kanisa hilo hawakuendelea lakini Kanisa linasimama na kufikisha miaka 25.

Katika maadhimisho hayo yalikuwa na maandamano ya kumtukuza Mungu pamoja na kuangaza amani ya nchi.Nae Mchungaji wa Kanisa hilo Emelda Maboya amesema kwa hatua walifikia wanamshikuru Mungu katika kusimamisha injili katika Kanisa hilo.

Amesema haikuwa kazi ndogo katika kujitoa kwa waumini katika Ujenzi wa Kanisa pamoja na wachungaji na maaskofu kutangaza neno la Mungu.

Kwa upande wa Askofu Msaidizi wa Jimbo la Dar es Salaam wa Kanisa hilo Jonathan Shemhambu amesema kuwa miaka 25 ya Kanisa ni neema ya Mungu kwani walianza wakati Mugumu katika kufikisha neno la Mungu lakini sasa matokeo yamekuwa mazuri katika kujenga imani kwa waumini.
 Waumini wa Kanisa la Calvary Assemblies of God wakiwa katika maandamano Jubilee ya Miaka 25  ya Kanisa hilo  Ubungo jijini Dar es Salaam.
 Askofu Mkuu wa Kanisa la Calvary Assemblies of God (C.A.G) Ubungo Dunstan Maboya akizungumza katika ibada ya Jubilee ya Miaka 25 ya Kanisa hilo jijini Dar es Salaam.
 Askofu Msaidizi wa Kanisa la Calvary Assemblies of God (C.A.G) Jonathan Shemhambu akizungumza namna walivyotumikia katika kutangaza injili ya Mungu katika Kanisa hilo hadi kufikia Jubilee ya Miaka 25.
Mchungaji wa Kanisa la Calvary Assemblies of God (C.A.G) Emelda Maboya akitoa maelezo kuhusiana na Jubilee ya Miaka 25 ya Kanisa hilo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...