Na Jusline Marco:Arusha

Serikali imeombwa kuweka uwiano wa wanafunzi wenye ufaulu wa daraja la kwanza katika shule zote za elimu ya juu ili kuleta motisha kwa wanafunzi wanaojiunga na masomo kwenye shule hizo.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkuu wa shule ya sekondari ya Mwandeti iliyopo katika kata ya Mwandeti,Wilayani Arumeru Mkoani Arusha kufuatia shule hiyo kushika nafasi ya nne kitaifa na nafasi ya pili kimkoa katika matokeo ya mtihani wa kidato cha sita.

Amesema kuwa pamoja na shule hiyo kutoa wanafunzi 70 wenye ufaulu wa daraja la kwanza na wanafunzi 6 wenye ufaulu wa daraja la pili jitihada kubwa zimetumika ili kufanikisha shule hiyo inafanya vizuri zaidi kwani wengi wao walijiunga wakiwa na ufaulu wa daraja la tatu na daraja la pili katika matokeo ya kidato cha nne.

Vilevile ameeleza kuwa kushika kwa nafasi hiyo kunatokana na jitihada kubwa zilizofanyika na uongozi wa shule hiyo kwa kushirikiana na walimu wao kutumia mbinu mbalimbali za ufundishaji pamoja na kufanya ziara za kimasomo katika shule mbalimbali nchini.

Pamoja na hayo baadhi ya changamoto zilizopo katika kata hiyo zimeoneka kukithiri kwa muda mrefu ikiwemo ubovu wa barabara ambayo huleta madhara makubwa kipindi cha mvua kutokana na miundombinu hiyo kutokarabatiwa na uongozi husika.

Kwa upande wake Mwalimu wa taaluma shuleni hapo Peter Saiguran amesema kuwa ufaulu huo umetokana na misingi waliyojiwekea ya ushirikiano wa walimu kwa walimu,uongozi shule hiyo na shule za jirani,walimu na wanafunzi pamoja uwepo wa maziringira rafiki ya madarasa ba mabweni kwa wanafunzi.

Sambamba na hayo ameeleza kuwa kutokana na kampeni za kuzuia ndoa na mimba za utotoni kwa watoto wa kike zilizofanywa na shule hiyo katika jamii ya kifugaji ya kimaasai kwa kuwataka wazazi kuwekeza elimu kwa watoto wao imechangi kwa kiwango kikubwa kuongezeka kwa kiwango cha ufaulu shuleni hapo.
Mkuu wa shule ya sekondari  Mwandeti John Masaawe iliyopo katika Kata ya Mwandeti,Wikayani Arumeru Mkoani Arusha iliyoshika nafasi ya nne kitaifa katika matokeo ya kidato cha sita.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...