Na Woinde Shizza Michuzi TV,Arusha

SERIKALI imesema imeridhishwa na kasi ya wakandarasi wanaojenga mradi wa ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme ,Kenya-Tanzania Power Interconnection (KTIPIP)ZTK wa kilovolti 400 inayopita Singida, Babati, Arusha hadi Namanga kwani unaenda mbio na mpaka sasa ujenzi umefanyika umekamilika kwa asilimia 51.

Hayo yamesemwa na Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu Mhandisi Innocent Luoga wakati akihitimisha ziara yake ya kukagua hatua iliofikia katika ujenzi wa njia ya umeme wa msongo wa kilovolti 400.Ziara hiyo ilihusisha kukagua njia ya umeme ya Namanga ,kituo cha kupoozea umeme 
cha Legur kilichopo ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Arumeru na njia za kusafirishia umeme zilizopo katika halmashauri ya Babati Vijijini katika kijiji cha Nagwa .

Amebainisha kuwa kazi zinazofanywa na wakandarasi waliopewa miradi hiyo ameridhishwa nazo kwani hadi sasa wameshafanya kazi kwa asilimia 51 na hivyo kubakisha asilimia 49 na anaamini kwa kasi wakandasi hao wanayoendelea nayo watakamilisha mradi huo kwa wakati uliopangwa. "Mradi huu unatakiwa kukamilika na kukabidhiwa rasmi kwa Serikali Aprili 2020".

Ameongeza kuwa "Nimepita na kuangalia hatua iliyofikiwa katika mradi huu wa njia ya usafirishaji wa umeme ambao miundombinu yake itaunganishwa katika vyanzo vya uzalishaji umeme.Nia ya ziara hii ni kuangalia tumefikia wapi hadi sasa hivi na kunachangamoto zipi zinazoukabili ili kama zipo Serikali itatue haraka na kazi iendelee." 

Pia amesema katika mradi huo kuna Lot T5 ambayo ya kwanza inaanzia Singira mpaka Babati na Lot T2 ya pili inaanzia Singida hadi Arusha na Lot T3 ya tatu inaanzia Arusha mpaka Namanga ,Lot T4 inausisha ujenzi wa vituo vya kupooza umeme ambapo kimoja kiko kisongo na kingine kitakuwepo pale Singida na Lot T5 itahusisha kusambaza umeme katika vijiji vyote vinavyopitiwa na mradi huo.

Amesema kulingana na kasi ambayo wakandaras hao wanaendanayo kunauwezekano mkubwa wa mradi huu kukamilika kabla ya ratiba iliyopangwa au utakamilika kwa wakati .“ Serikali tumewaagiza wakandarasi hawa wafanye kazi kila siku,wakandarasi wawatumie vijana wetu katika kazi zote kazi ambazo zinaitaji elimu na hata zile ambazo hazihitaji elimu na katika suala hili nawapongeza wakandarasi maana wametii maelekezo.

"Wameajiri vijana zaidi ya 400 ambao wanatoka katika vijiji ambavyo miradi imepita kuanzia pale ulipoanzia Namanga hadi Singida.Pia tumewataka wakandarasi washirikiane na jamii zinazozunguka 
miradi hii ili kusiwepo na changamoto,"amesema.

Kwa upande wake Mratibu na Msimamizi wa Mradi huo kutoka Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Mhandisi Peter Kigadye amewataka wananchi waendelee kutoa ushirikiano kwa wakandarasi hao ikiwa ni pamoja na kuwasadia kazi mbalimbali za ujenzi.

Pia Serikali imewahaidi wakandarasi hao kuwasaida katika masuala mbalimbali ikiwemo wakati wa vitu kutoa vifaa vya ujenzi bandarini ili wakamilishe mradi huo kwa wakati na kwamba mradi huo utakamapokamilika utachochea maendeleo katika nchi yetu. 
Muendesha mashine ya kuchanganya sege kutoka kampuni ya ukandarasi ya Booygues , Dominic Heriman akimuonyesha Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Innocent Luoga jinsi wanavyochanganya sege kwa kutumia komputa wakati katibu alipofanya ziara yake ya kukagua hatua iliofikia katika ujenzi wa njia ya umeme wa msongo wa kilovolti 400 hapo ni ndani ya store yard ya Lot T2 iliopo katika kijiji cha Nanja . 

 Meneja wa mradi  kutoka kampuni ya Booygues Energies &services Potier Mathiew  akitoa maelekezo kwa  Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Innocent Luoga pamoja na mratibu na Msimamizi wa Mradi huo kutoka Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Mhandisi Peter Kigadye pamoja na viongozi mbalimbali wa Tanesco wakiwemo wakandarasi wakati walipotembelea moja ya shimo lililopo tayari kwa ajili ya kusimamisha mnara. 
Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Innocent Luoga akitoa maelekezo kwa mkandarasi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...