Na.Khadija Seif, Michuzi TV

KAMPUNI ya kuuza na kusambaza filamu mtandaoni (SWAHILIFLIX) imepania kuwapa kipaumbele wasanii kutengeneza kazi zenye ubora ili kijitangaza duniani.

Akizungumza na wanahabari jijini Dar es salaam (pichani chini) muwakilishi kutoka Kampuni ya Swahiliflix Nazir Atul amesema kutokana na kukua kwa teknolojia katika utandawazi katika kila sekta shughuli nyingi zinafanywa na mitandao ili kusaidia kufikia mahitaji ya watumiaji.

"Kwa sasa wapenzi,mashabiki ,wakereketwa wa tasnia ya filamu wataona  filamu wazipendazo kupitia Swahiliflix kwa haraka na kwa nafuu ,"

Pia Atul amesema rasmi Kampuni hiyo inatarajia kufanya uzinduzi julai 31 mwaka huu katika ukumbi wa Mlimani city jijini Dar es salaam. 

Kwa upande wake Msanii wa Bongomovie nchini Aunt Ezekiel  amesema wakati mwengine wasanii wamekua wakiboresha,kukuza sanaa kwa pamoja na kujitahidi kuwa tofauti lakini bado changamoto inabaki katika upatikanaji wa soko la kuuza kazi zao.

"Wadau wa filamu ni wakati wa kuburudika na filamu za kitanzania viganjwani mwao kupitia Swahiliflix, kwani imekua changamoto sana kwa shabiki kuhitaji kazi zako kupitia mtandao wa youtube na muda mwingine haipati kazi yako ikiwa kamili ,"

Aidha,Mkwere ameeleza hapo awali kulikua na tatizo la wasanii wakongwe kutoonekana kwenye kazi mpya kutokana na kukosekana kwa wadau  wanaosambaza na kuuza kazi za sanaa .

"Swahiliflix italeta Mapinduzi ya tasnia ya filamu kutokana na kazi zetu kuzitangaza zenyewe mtandaoni na wadau kutokana na kuwepo kwa Swahiliflix kuleta chachu na mabadiliko makubwa kwa wasanii kurudi kwa wingi,"

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...