Ubalozi wa Shirikisho la Jamuhuri ya Brazil Zanzibar unapenda kuwatarifu wote kuwa ujumbe wa Tanzania uliojumuisha wafanyabiashara 12 kutoka sekta binafsi na baadhi ya wakuu wa mashirika ya umma waliokwenda kwenye ziara ya kibiashara nchini Brazil kwa siku kumi unatarajiwa kurudi nchini Tanzania kesho Jumatatu saa tisa kamili mchana kupitia uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere Airport na ndege ya South African Aiways ukitokea nchini Brazil.

Ziara hii ilianza tarehe 28 Juni hadi 08 Julai,2019 yenye lengo la kutafuta fursa za kibiashara, uwekezaji na masoko kwa bidhaa zinozalishwa Tanzania ukiongozwa na Balozi wa Heshima wa Shirikisho la Jamuhuri ya Brazil Zanzibar Mhe. Abdulsamad Abdulrahim

The Consulate of Brazil Zanzibar avails itself the assurances of its highest consideration.

The Honorary Consulate of the Federative Republic of Brazil, Zanzibar

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...