Taasisi ya
Young Scientists Tanzania(YST) inatarajia kufanya maonyesho ya Wanasayansi
chipukizi kuanzia Julai 31 mpaka adosti 1 katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
na Waandishi wa habari mapema leo jijini Dar es Salaam Mwneyekiti w abodi ya
YST nchini Profesa Yunus Mgaya amesema kuwa wanafunzi wanaopata fursa ya
kushiriki maonyesho aya walipata fursa ya kuboresha ujuzi wao wa kisayansi
kupitia mango wa uwezeshaji ulioendeshwa na wanasayansi washauri .
"kwa
siku mbili wanasayansi chipukizi wataonyesha kazi zao katika nyanja mbalimbali
za sayansi kama kemia, fizikia na hesabu ,biology mazingira na sayansi ya jamii
na tekonolojia ,kazi hizi za kisayansi hasa ziwe zimejikitakatika utatuzi wa
matatizo katika afya ,Kilimo, usalama wa chakula ,mawasiliano na usafirishaji
" Amesema Prof Mgaya.
amesema
wanasayansi watakaokuwa na ugunduzi mzuri watazawadiwa pesa taslim na medali
wanasayansi wanne watapewa udhamini wa kusoma chuo kikuu na shirika la Karim
mjee Jivanjee Foundaton.
Washindi
wa jumla wataiwakilisha Tanzania kwenye Maonesho ya kimataifa ya Eskom Expo
Young Scientists jijini Johannesburg Afrika Kusuni Oktoba mwaka huu.
Mwenyekiti wa bodi wa Tasisi ya Young Scientists Tanzania(YST), Prof Yunus Mgaya akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam juu ya kilele cha Maonesho ya tisa ya wanasayansi chipukizi yatakayofanyika katika ukumbi wa Julius Nyerere Convention Centre kuanzia Julai 31 mpaka Agosti 1 mwaka 2019.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)
Mwanzilishi Mwenza wa YST Nchini Dr.Gosbert Kamugisha (katikati) akieleza namna wanafunzi walioshiriki katika maonyesho hayo katika kipindi cha nyuma fursa walizopata ikiwemo ufadhili wa masomo ya kusoma elimu ya juu nje ya nchi.kushoto Mwenyekiti wa bodi wa Tasisi ya Young Scientists Tanzania(YST), Prof Yunus Mgaya kulia ni Mwanzilishi wa YST,Joseph Clowry.
waandishi wa habari wakimsiliza Mwenyekiti wa bodi wa Tasisi ya Young Scientists Tanzania(YST), Prof Yunus Mgaya.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...