Anaandika Abdullatif Yunus Michuzi TV. Kagera.

Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) inazidi kuweka mazingira mazuri ya kuhakikisha Mkulima hasa Mkulima wa zao la Kahawa Mkoani Kagera, ananufaika na Kilimo cha zao hilo ambapo Benki hiyo kwa kushirikiana na Wadau mbalimbali wametambulisha rasmi mfumo jumuishi utakaomsaidia Mkulima wa zao la Kahawa kupata huduma za kifedha.

Mfumo huu ni shirikishi kupitia Vyama vya ushirika (AMCOS) ambavyo vyama hivi vinamtambua Mkulima wa eneo husika, ukiwa na lengo la kuwawezesha wadau kumfikia mkulima kwa urahisi ili kumsogezea huduma mbalimbali za kifedha ikiwemo bei ya mazao, bima za afya na mikopo ya pembejeo kirahisi.

Mfumo Jumuishi unaowashirikisha wadau wa wa sekta ya fedha na mawasiliano zikiwemo Benki, mitandao ya Simu, Mfuko wa Bima, Wizara ya fedha, na wengineo, utamsaidia Mkulima katika kuhakikisha anapata Soko la uhakika, kujua bei ya soko, kuwa na mfumo wa kupata bei nzuri ya mazao, kulipwa fedha take yote kwa wakati na urahisi, kujikimu kimaisha na kiafya yeye na familia yake, kuwa mwekezaji kwenye Tanzania ya Viwanda, kuwa na fursa nyingi za kuwekeza kwa baadae na pia kumhakikishia Mkulima usalama wa fedha zake.

Mfumo jumuishi ni mpango wa wadau chini ya Benki ya Kilimo, kumuendea Mkulima kwa pamoja ambapo awali kila mdau alikuwa akimfuata Mkulima kwa njia zake, lakini lengo kubwa ni kumuondolea Mkulima Usumbufu na kuwa Tegemezi.

Tayari Mfumo jumuishi umeanzishwa na kufanikiwa katika zao la Korosho kwa Mikoa ya Kusini, Lindi Mtwara na Ruvuma, na sasa unatambulishwa rasmi kwa Mikoa ya Kanda ya ziwa kwa Kuanzia Kagera.
 Bwana Kazilahabi Jumanne Kaimu Meneja Benki ya maendeleo ya  Kilimo Kanda ya Ziwa akizungumza na vyombo vya habari juu ya Kampeni ya  mfumo Jumuishi iliyoanza Rasmi Mkoani Kagera.
 Pichani Kahawa iliyokobolewa baada ya kukusanywa na Vyama vya Msingi huko Wilayani, huletwa KCU kwa ajili ya hatua nyingine.
Pichani ni Ndg Kazilahabi Jumanne Kaimu Meneja Benki ya Wakulima Kanda ya Ziwa, akikagua Kahawa Iliyokobolewa tayari kwa hatua nyingine, kama alivyokutwa na Kamera yetu Ofisi za Chama kikuu cha Ushirika KCU 1990 ltd.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...