Na Woinde Shizza Michuzi Tv,Arusha

Tanzania ina Upungufu wa Tani zipatazo 350,000 za Samaki kwa mwaka huku mahitaji yakiwa ni Tani 700,000 ambapo kwa mwaka kiasi cha tani 350,000 kinazalishwa,hivyo watanzania wametakiwa kuchangamkia fursa ya uzalishaji ili kufikia malengo ya mahitaji ya samaki.

Kauli hiyo imeelezwa jijini Arusha na Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega wakati wa kutiliana saini makubaliano ya mashirikiano baina ya serikali ya Tanzania na nchi ya Uholanzi katika Nyanja za maendeleo ya ufugaji wa Samaki na Kuku.

Ulega amesema kuwa ushirikiano huo wa kimaendeleo na nchi ya Uholanzi umefikia miaka zaidi ya 40 katika njanja mbali mbali,ikiwemo kilimo cha Mboga mboga,Viazi Mviringo, Ufugaji wa kuku na Samaki yanayosaidia kuongeza uzalishaji wa protini na mapato kwa Taifa kwa ujumla.

Amesema kuwa Tanzania inauhitaji mkubwa wa protini inayotokana na samaki na kuku ndio maana wamekubaliana na Taifa hilo la uholanzi kuweza kuboresha Nyanja hizo kwa lengo la kutoa elimu kwa wafugaji na wakulima wa mazao ya samaki.

“Kama nchi tumejipanga kuhakikisha ukuaji wa sekta ya ufugaji wa Samaki na kuku unakuwa kwa kiasi kikubwa kuongeza Pato la taifa kutoka asilimia 9 tunazochangia katika pato la taifa”

Amesema serikali itaendelea kushirikiana na sekta binafsi katika kuhakikisha kwamba Uzalishaji wa kuku na Ufugaji wa samaki unaboreshwa na kuona viwanda vya kuchakata mazao hayo kuondoa changamoto mbali mbali ili kufikia malengo ya uzalishaji na kuondoa upungufu wa uhitaji wa soko.
Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega Ulega pamoja na Naibu Waziri wa Kilimo maliasili na Usalama wa Chakula Bi Marjolyn Sonnema kutoka nchini Uholanzi wakitia saini makubaliano ya mashirikiano baina ya serikali ya Tanzania na nchi ya Uholanzi katika Nyanja za maendeleo ya ufugaji wa Samaki na Kuku (picha na Woinde Shizza,Arusha).
Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega Ulega pamoja na Naibu Waziri wa Kilimo maliasili na Usalama wa Chakula Bi Marjolyn Sonnema kutoka nchini Uholanzi wakibadilishana nyaraka mara baada ya kutia saini.
Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega Ulegaakiongea na waandishi wa habari mara baada ya kutia saini nyaraka hizo za makuliano mashirikiano baina ya serikali ya Tanzania na nchi ya Uholanzi katika Nyanja za maendeleo ya ufugaji wa Samaki na Kuku .
Naibu Waziri wa Kilimo maliasili na Usalama wa Chakula Bi Marjolyn Sonnema kutoka nchini Uholanzi akimkabidhi Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo na Mifugo, Elisante Ole Gabriel zawadi ambayo wametoka nayo nchini uholanzi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...