Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara ya TIB Corporate Bank Ltd (TIB CBL) Fred Luvanda akizungumza na waandishi wa habari na kutolea ufafanuzi wa Benki Kuu (BOT) kumuondoa aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo pamoja na kuwaondoa hofu wateja na wadau wote wa benki ya Biashara TIB na wananchi kwa ujumla.

Na Zainab Nyamka, Michuzi TV
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara ya TIB Corporate Bank Ltd (TIB CBL) Fred Luvanda ametolea ufafanuzi wa Benki Kuu (BOT) kuondolewa kwa aliyekuwa Mtendaji mkuu wa benki hiyo  Frank Nyabundege.
Akizungumza na waandishi wa habari, Luvanda amesema kuwa kuna sababu nyingi ambazo zinaweza kupelekea kwa BOT kufanya maamuzi ya kuichukua benki inayoshindwa kulinda amana za wateja na kuiweka chini ya mamlaka yake.
Luvanda ameeleza, Benki ya TIB Corporate haiko chini ya usimamizi wa mabenki bali ni mabadiliko ya uongozi wa juu tu kwa kuondolewa kwa Mkurugenzi Mtendaji  ila Benki ya TIB Corporate inaendelea kuhudumia wateja wake kama kawaida kwa ubora na ufanisi wa hali ya juu chini ya menejimenti na bodi ya wakurugenzi iliyokuwapo awali.

Benki kuu ilichukua uamuzi huo chini ya mamlaka iliyopewa kwa mujibu wa kifungu cha sheria namba 33(1) na 33(2)(f)  pamoja na 33 (2)(b)cha sheria ya Mabenki  na Taasisi za fedha ya mwaka 2006," 

Nachukua nafasi hii kuwatoa wasiwasi wateja na wadau wote wa benki ya Biashara TIB na wananchi kwa ujumla, wajue kuwa  huduma zinaendelea kama kawaida, pia mfahamu  kuwa Serikali na Benki kuu inatambua umuhimu wa Benki hii hivyo itaendelea kutoa ushirikiano wa karibu ili kuhakikisha Benki  inazidi kuboresha huduma zake na kukua kwa maendeleo ya nchi yetu.

TIB ni Benki ya  biashara inayomilikiwa na Serikali. Benki inatoa huduma zote za kibenki za kibishara kwa  mashirika na taasisi za aina mbalimbali za serikali na  binafsi ,pia benki inatoa huduma kwa watu binafsi. Benki ina matawi 7 kwa sasa,  Dar es salaam (3), Mwanza , Arusha,  Mbeya na Dodoma

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...