Katika kutimiza azma ya kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025, Serikali inaendelea, pamoja na mambo mengine, kuimarisha mazingira ya uwekezaji na ufanyaji biashara katika sekta mbali mbali hapa nchini, ikiwemo sekta ya usafirishaji. Sekta hii ni miongoni mwa Sekta zenye mchango mkubwa katika kukuza uchumi na kuongeza mapato ya Serikali. 

Aidha, sekta hii imekuwa ikichangia pia kuzalisha ajira kwa vijana wetu katika nafasi mbali mbali kama vile Madereva, Mafundi na kada nyingine nyingi.  Pamoja na mchango mkubwa unaotolewa na sekta hii, zipo changamoto kadhaa ambazo zinahitaji kufanyiwa kazi na Serikali kwa kushirikiana na wadau. 

Kwa upande wa utekelezaji wa Sheria za Kazi, changamoto zimeendelea kujitokeza katika masuala ya Mikataba ya Ajira, Malipo ya Mishahara na Posho mbali mbali, ambapo imebainika yapo Makampuni machache yanayolenga kuchafua kazi nzuri inayofanywa na sekta hii, ambapo makampuni hayo machache yamekuwa yakifanya udanganyifu kwenye Mikataba ya Ajira za Madereva wao pindi yanapofanya maombi ya Leseni za Usafirishaji. 

Aidha, katika jitihada za kuzipatia ufumbuzi changamoto hizo, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi; Kitengo cha Usalama Barabarani na LATRA inatarajia kufanya Zoezi Maalum la  Ukaguzi kwa lengo la kukagua Mikataba hiyo na kuangalia utekelezaji wa Sheria kwa ujumla. 

Zoezi hili linatarajiwa kufanyika kwa namna mbili tofauti ambapo; (i) Maafisa Kaziwaliopo katika Ofisi za Kazi watapita katika Kampuni zote za Usafirishaji na (ii)Timu maalum ya Maafisa Kazi wa kushirikiana na Viongozi wa Vyama vyaWafanyakazi Madereva, LATRA na Jeshi la Polisi; Kitengo cha UsalamaBarabarani watafanya Ukaguzi wa Mikataba kwenye Vituo Vikuu vya Ukaguzikama vile Kituo cha Mabasi Ubungo, Kituo cha Kuegesha Malori chaMisugusugu na vituo vingine vinavyofanana na hivyo hapa nchini. 

Aidha, sambamba na ukaguzi huo, Viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi
Madereva na Vyama vya Waajiri watapatiwa elimu kuhusu haki na wajibu waokatika kutekeleza Sheria za Kazi. 

Hivyo, ninapenda kuwaarifu Wamiliki wa Vyombo vya Usafirishaji, WafanyakaziMadereva na Umma kwa ujumla kuwa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajirana Wenye Ulemavu inatarajia kuanza rasmi Zoezi la Ukaguzi wa Mikataba yaAjira ya Madereva na Utekelezaji wa Sheria za Kazi kwa ujumla ifikapo tarehe 15Julai, 2019. 

Ili kulifanya zoezi hili kuwa lenye ufanisi, ni vema Wamiliki wa Vyombo vya
Usafirishaji kuhakikisha kuwa Mikataba ya Madereva wenu inakuwepo katikamaeneo yenu ya kazi, na kwa upande wa Madereva, kuhakikisha mnakuwa nanakala za Mikataba yenu mnapokuwa katika kazi zenu ili iwe rahisi kwaWakaguzi kuiona. 

Aidha, ninapenda kuwaarifu kuwa Zoezi la Ukaguzi wa Mikataba ya ajira na
Utekelezaji wa Sheria kwa ujumla litakuwa endelevu na litaendelea pia katikaSekta nyingine hapa nchini. 

Mwisho, ninapenda kutoa wito kwa Wamiliki wa Vyombo vya Usafirishaji,
Viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi Madereva pamoja na Madereva wote
nchini kutoa ushirikiano wa kutosha kwa Wakaguzi wakati wote wa utekelezajiwa zoezi hili ili kutoathiri utoaji wa huduma kwa wananchi kwa namna yoyote ile.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...