Na Said Mwishehe, Michuzi TV-Morogoro

WAANDISHI wa Habari nchini Tanzania wametakiwa kuibua masuala ya kimkakati katika kuitangaza nchi kimataifa, hasa kwa manufaa ya kiuchumi, kisiasa na kitamaduni

Hayo yameelezwa mkoani Morogoro jana na Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Dk. Ayoub Rioba wakati akitoa mada kwa wanahabari waliohudhuria semina ya maandalizi ya mkutano wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).

Dk Rioba, amesema yapo masuala mengi yanayohitaji kuripotiwa kizalendo kwa kuwa hakuna taifa linaloweza kuiinua Tanzania kitamaduni bali Tanzania yenyewe

“Mimi nimewahi kuishi nchi mbalimbali duniani, nimefanya kazia na kusoma katika maeneo mbalimbali ya dunia, sijawahi kuona habari za kwetu zikipewa kipaumbele. Kwa mfano nikiwa Ulaya sikuona habari za mataifa ya Afrika, labda kutokee habati za vita au magonjwa.

“Hivyo, tunatakiwa kuzingatia ni kitu gani tunakipeleka kwa watazamaji na wasomaji wetu. Tujipange kwa ajili ya kujitangaza, kazi hii haiwezi kufanywa na mwengine zaidi ya nyinyi wanahabari,” alisema Dk. Rioba.

Kwa upande wake, Hebert Mrango ambaye kwa nyakati tofauti ameitumikia Serikali ya Tanzania kwenye masuala ya kitaifa, kidiplomasia na kimataifa; wakati akitoa mada alisema vijana wengi kwa sasa huenda hawajui mantiki ya SADC.

Hivyo, ipo haja ya kusoma nyaraka nyingi ili kuujua msingi wa kuanzishwa jumuiya hii. Ambapo Tanzania ina mchango mkubwa katika uanzishwaji wake.“SADC ilianzishwa kwa ajili ya maendeleo endelevu, kwa mfano tulikuwa na makubaliano kuwa hadi ikifika mwaka 2008 iwe asilimia Zaidi ya 80 ya bidhaa zitakazouzwa ndani ya nchi wanachama ziondolewe kodi

“Hii ingeweza kutusaidia kuondokana na utegemezi katika mataifa mengine ya Ulaya, lakini kuna baadhi ya masuala yalikuwa magumu kufuatwa katika uondoaji kodi hasa bidhaa za kimkakati zikizokuwa zikizalishwa katika nchi wanachama ambazo zilikuwa tegemezi la kiuchumi kwa mataifa yao,” amesema Balozi Mrango.

Awali, akieleza lengo la kufanyika semina hiyo ya siku tatu ambayo ni awamu ya pili, Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, Zamaradi Kawawa alisema anaamini waandishi waliopikwa katika semina hiyo watakuwa mabalozi wazuri hata baada ya kustaafu kazi ya uandishi.

“Tunataka muwe na uelewa mpana juu ya suala hili la SADC, si kwa ajili ya vikao tu vitakavyofanyika mwezi ujao lakini hata kuwa na elimu ya kutosha hata kuwasaidia wengine. Tunaamini SADC itaandikwa sana kwa kipindi hiki,” amesema Kawawa.

Kwa mwaka huu SADC itakuwa na vikao vyake nchini katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere (JNICC), kati ya Agosti 17 na 18.

Aidha, kabla yah apo mapema mwezi ujao kuanzia Agosti 5 hadi Agosti 8, mwaka huu kutakuwa na mapnyesho ya viwanda katika ukumbi wa JNICC, Agosti 9 vitaanza vikao vingine vya SADC vikianza na vikao vya kamati, vikao vya mawaziri wa mambo ya nje kwa nchi wanachama, vikao vya makatibu wakuu katika nchi wanachama na wakurugenzi kisha ndio mkutano mkuu ambao utakutanisha viongozi wan chi kwa siku mbili Agosti 17 na 18.

Mara ya mwisho vikao hivi kufanyika Tanzania ilikuwa mwaka 2003 katika Serikali ya Awamu ya Tatu chini ya Rais Benjamin Mkapa.

SADC ina nchi wanachama 16 ambazo ni: Tanzania, Malawi, Angola, Zimbabwe, Msumbiji, Afrika Kusini, Ushelisheli, Zambia, Eswatini, Commoro, Botswana, Lesotho, Madagascar, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Mauritius na Namibia.
Mkuu wa Operesheni na Mafunzo, Brigedi ya Magharibi, Jeshi la Ulinzi la
Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Kanali Wilbert A. Ibuge akiwasilisha mada wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa weledi katika kuandika na kuripoti habari zinazohusu Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) yanayoendelea mjini Morogoro leo Julai 12, 2019 ikiwa ni siku ya pili ya mafunzo hayo kwa kundi la pili la waandishi hao. 
Sehemu ya washiriki wa mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa weledi katika kuandika na kuripoti habari zinazohusu Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika yanayoendelea mjini orogoro leo Julai 12, 2019 ikiwa ni siku ya pili ya mafunzo hayo 
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari- MAELEZO Bi. Zamaradi Kawawa
akizungumza wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa weledi katika kuandika na kuripoti habari zinazohusu Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) yanayoendelea mjini Morogoro leo Julai 12, 2019 ikiwa ni siku ya pili ya mafunzo hayo kwa waandishi hao.Mmoja wa washiriki wa mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari ili waweze kuandika na kuripoti habari za SADC kwa weledi Bw. Henry Mabumo akieleza jinsi Tanzania inavyoweza kunufaika na Jumuiya hiyo kupitia fursa zilizopo katika nchi wanachama, hayo yamejiri leo Julai 12, 2019 mjini Morogoro wakati wa siku ya pili ya mafunzo kwa waandishi hao. 
Katibu Mkuu mstaafu Balozi Hebert Mrango akisisitiza jambo wakati wa
mafunzo kwa kundi la pili la waandishi wa habari wanaojengewa uwezo ili waweze wa kuandika na kuripoti habari za nchi wanachama wa SADC, hayo yamejiri mjini Morogoro Julai 12, 2019 ambapo mafunzo ya kundi la pili kwa waandishi hao yanafanyika kwa siku tatu.
Katibu Mkuu mstaafu Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Mussa Uledi akijibu hoja
mbalimbali za waandishi wa habari walioshiriki mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa weledi katika kuandika na kuripoti habari zinazohusu Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) yanayoendelea mjini Morogoro leo Julai 12, 2019 ikiwa ni siku ya pili ya mafunzo hayo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...