Jeshi la Zimamoto na Uokoaji linapenda kuutaarifu Umma
wa Tanzania kwamba, Wamiliki wa majengo na
Wafanyabiashara waliofanyiwa ukaguzi wa kinga na tahadhari dhidi ya majanga ya
moto na kukidhi vigezo vya usalama wa
moto, kufika au kuwasiliana na Ofisi ya Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na
Uokoaji Mkoa husika au kituo cha Jeshi hilo kilicho karibu yake, kwa ajili ya kuchukua Hati ya Usalama dhidi ya Moto (Fire Safety Certificate).
Cheti cha Usalama dhidi ya Moto kinapatikana baada ya
kufanyiwa ukaguzi wa kinga na tahadhari dhidi ya majanga kwenye majengo.
Ukaguzi huo unafanyika kwa mujibu wa Sheria namba 14 ya mwaka 2007, ikisomwa pamoja na Kanuni ya Vyeti na Usalama wa
moto ya Mwaka 2008 na marekebisho ya mwaka 2014 (Fire and Rescue
Force Safety Inspections and Certificates Regulations of 2008 GN.106 and its Amendment
GN 63 of 2014.) Pamoja na Kanuni ya tahadhari dhidi ya moto kwenye majengo
ya mwaka 2015 (Fire and Rescue Force Fire
Safety Precaution in Building Regulations of 2015 GN 516.)
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji linatoa rai kwa Umma
kujenga tabia ya kutembelea vituo vilivyo karibu kwa ajili ya kupata ushauri
pamoja na kuchukua hati za usalama dhidi ya moto.
Imetolewa na,
Kitengo cha Habari, Uhusiano na Elimu kwa Umma Jeshi
la Zimamoto na Uokoaji,
Makao Makuu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...