Kaimu Mkuu was Chuo Cha Mtakatifu Joseph( SJUIT), Prof. Innocent Ngalinda akizungumza , wakati akiwaaga wanafunzi watano kati ya 80 wa Stadhahada ya Uhandisi wa Sayansi ya Komputa, wanaoenda nchini India kwa ajili ya kumalizia mwaka wa mwisho
Mkuu wa Chuo chaMtakatifu Joseph( SJUIT), Prof. Innocent Ngalinda, akitoa neno la mwisho kwa Wanafunzi wanaosafiri.
Mwanafunzi wa Kike aliyepata nafasi ya kwenda India kusoma Masomo ya Uhandisi wa Kompyuta ,Sky Karoli akizungumza na Waandishi wa Habari.
Mwanafunzi wa Kiume George Temu aakifafanua kwa Waandishi wa habari umuhimu wa kwenda kusoma India.

Na Humphrey Shao, Michuzi Tv

WANAFUNZI wanaopata ufadhili wa kwenda kusoma nje ya nchi, wametakiwa kujiepusha na shughuli za kufanya vibarua katika nchi za watu kwa lengo la kujipatia kipato na badala yake wazingatie kile kilichowapeleka.

Wito huo umetolewa na Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Joseph( SJUIT), Prof. Innocent Ngalinda, wakati akiwaaga wanafunzi watano kati ya 80 wa Stadhahada ya Uhandisi wa Sayansi ya Komputa, wanaoenda nchini India kwa ajili ya kumalizia mwaka wa mwisho wa masomo yao kwa lengo la kuwaongezea ufanisi katika taaluma hiyo.

Alisema kila mwaka chuo hicho kimekuwa kikiwapeleka wanafunzi wote wa mwaka wa mwisho ngazi ya Stadhahada na Shahada wa Uhandisi wa Sanyasi ya Komputa nchini India kwa ajili ya kumalizia masomo yao ili wapate uzoefu wa kuendana na teknolojia ya masomo hayo.

"Nina waasa, chuo kinawapeleka India kwa ajili ya kupata elimu, kuongeza taaluma ili kuwa wahitimu mnaoendana na teknolojia ya Sayansi ya Komputa, acheni kwenda kufanya kazi za vibarua, acheni kwenda kufanya uhuni na mambo ambayo hayaendani na kilichowapeleka kazi yenu iwe kusoma na mrejee nchini mkiwa mmepata elimu na si vinginevyo," alisema Prof. Ngalinda.

Alisema kumekuwapo na tabia za vijana wanaokwenda katika nchi mbalimbali duniani kwa ajili ya masomo kujihusisha na vitendo visivyo na maadili na matokeo yake kuharibu mipango yao na malengo tayariwa.

Aidha, alisema chuo hicho kinazingatia ubora wa elimu wanayotoa na ndio sababu wamekuwa wakipeleka wanafunzi nje ya nchi ili kuwapatia elimu inayoendana na ukuaji wa teknolojia na kukidhi matakwa ya soko la ajira nchini.

"Gharama za masomo wanayolipia ndizo zinazotumika kuwapeleka India kwa ajili ya kumalizia masomo yao na si kwamba tunawatoza fedha nyingine. Huu ni mkakati wa chuo kuhakikisha wanafunzi wanapata elimu iliyo bora na wala hakuna haja ya kusafiri kuifata mataifa mengine kwa sababu tunakidhi mahitaji yote," alisema.

Kwa upande wa wanafunzi wanaokwenda nchini India, Sky Karoli, mbali na kuushukuru uongozi wa chuo hicho kwa kuwawezesha kupata uzoefu kutoka chuo cha nchini India alisema ni fursa nzuri kwao.Alisema wanaamini watapata elimu iliyo bora itakayo wawezesha kuwa wahitimu wanaoweza kutatua changamoto zilizopo ndani ya jamii.

Naye George Temu, alisema wanaenda kujifunza namna nchi nyingine zilivyopiga hatua katika ukuaji wa teknolojia ili kupata elimu itakayowawezesha kuifanyia kazi wakirudi nchini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...