Mwezeshaji kutoka Wizara ya Afya,Zanzibar, Rukia Shani akiendelea kutoa mafunzo ya Usimamizi wa vimelea hatarishi vya kibaiolojia kwa wataalamu wa maabara wakati wa mafunzo hayo, yaliyowahusisha wataalamu hao kutoka sekta ya Afya ya Binadamu na Wanyama, Jijini Arusha, tarehe 29 Julai, 2019.
Baadhi ya wataalamu wa maabara wakifuatilia mafunzo ya Usimamizi wa vimelea hatarishi vya kibaiolojia wakati wa mafunzo hayo yaliyowahusisha wataalamu hao kutoka sekta ya Afya ya Binadamu na Wanyama, Jijini Arusha, tarehe 29 Julai, 2019.
Mratibu wa Afya Moja Kitaifa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Harrison Chinyuka, akieleza umuhimu wa mafunzo ya Usimamizi wa vimelea hatarishi vya kibaiolojia kwa wataalamu wa maabara wakatia akifungua mafunzo hayo yaliyowahusisha wataalamu hao kutoka sekta ya Afya ya Binadamu na Wanyama, Jijini Arusha, tarehe 29 Julai, 2019.
Mwezeshaji kutoka Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto akiendelea kutoa mafunzo ya Usimamizi wa vimelea hatarishi vya kibaiolojia kwa wataalamu wa maabara wakati wa mafunzo hayo, Jijini Arusha, tarehe 29 Julai, 2019.
Mshiriki wa mafunzo ya Usimamizi wa vimelea hatarishi vya kibaiolojia kwa wataalamu wa maabara, Basilius Kilowoko, akichangia wakati wa mafunzo hayo, Jijini Arusha, tarehe 29 Julai, 2019.
Mshiriki wa mafunzo ya Usimamizi wa vimelea hatarishi vya kibaiolojia kwa wataalamu wa maabara, Fredy Makoga, akichangia wakati wa mafunzo hayo, Jijini Arusha, tarehe 29 Julai, 2019.
Washiriki wa mafunzo ya Usimamizi wa vimelea hatarishi vya kibaiolojia kwa wataalamu wa maabara, wakiwa katika picha ya pamoja na Mratibu wa Afya Moja Kitaifa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Harrison Chinyuka (katikati walio kaa) mafunzo hayo yaliyowahusisha wataalamu hao kutoka sekta ya Afya ya Binadamu na Wanyama, Jijini Arusha, tarehe 29 Julai, 2019.




Na. OWM, ARUSHA

Wataalam wa maabara nchini kwa kutumia Dhana ya Afya moja ambao ni wataalam wa maabara kutoka sekta ya Afya ya binadamu, Afya ya wanyamapori na mifugo pamoja na mazingira wameendelea kupewa mafunzo ya Msingi ya Usimamizi na udhibiti wa vimelea hatarishi vya kibailojia kwa kuimarisha ulinzi na usalama wa sampuli za vimelea hivyo.

Vimelea hatarishi vya kibailojia vinaweza sambaza magonjwa kwa wanyama na binadamu iwapo ulinzi na usalama wake hautaimarishwa wakati wa kuvichukua kwa wanyama, binadamu na mimea au wakati wa kusafirisha vimelea hivyo na kuvipeleka maabara kwa ajili ya Uchunguzi pia wakati kuvifanyia uchunguzi pamoja na wakati wa kuviharibu mara baada ya kuvifanyia uchunguzi.

Akiongea wakati wa kufungua mafunzo hayo, leo tarehe 29, Julai, 2019, Mratibu wa Afya Moja Kitaifa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Harrison Chinyuka amefafanua kuwa Mafunzo hayo ni mwendelezo wa mafunzo ya msingi ambayo wataalam hao tayari walishafundishwa mafunzo ya awali ya Usimamizi na Usalama wa vimelea hatarishi vya kibailojia mnamo mwezi Machi, mwaka huu.

“Lengo la mafunzo haya ni kuiwezesha nchi yetu kuwa na wataalamu wa maabara wenye uelewa kuhusu dhana za vihatarishi vya kibaiolojia, ikiwemo wakati wa kusafirisha vimelea hivyo na kuvipeleka maabara kwa ajili ya Uchunguzi pia wakati kuvifanyia uchunguzi pamoja na wakati wa kuviharibu mara baada ya kuvifanyia uchunguzi” amesema Chinyuka

Wakiongea kwa nyakati tofauti washiriki wa mafunzo hayo wamebainisha kuwa baada ya mfunzo hayo, mienendo na matendo yao wakiwa maabara itazingatia usalama wa afya zao na usalama wa jamii inayowazunguka pamoja na Usalama wa watanzania, kwa kusimamia na kudhibiti vihatarishi vya kiulinzi na usalama vitokanavyo na vimelea hatarishi amabavyo wataalamu hao wamepewa dhamana ya kuvifanyia kazi.

Mafunzo hayo ya siku tano, yameandaliwa na DTRA na Sandia National Laboratories na wawezeshaji wa hapa nchini kutoka wizara ya Afya, maendeleo ya Jamii,Jinsia , Wazee na watoto pamoja na Wizara ya Uvuvi na Mifugo, chini ya Uratibu wa Ofisi ya Waziri Mkuu.

Afya Moja ni dhana ni dhana inayojumuisha sekta ya afya ya binadamu , wanyamapori, mifugo na mazingira katika kujiandaa , kufuatilia na kukabili magonjwa yanayoathiri binadamu ,wanyamapori na mifugo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...