MAMLAKA ya Hali ya Hewa nchini, (TMA) kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imeandaa mpango maalumu wenye lengo la kuongeza ufanisi wa utoaji wa tahadhari za hali mbaya ya hewa kwa watumiaji wa Ziwa Victoria.

Mpango huo umebainishwa leo Julai 18, 2019 na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA Dkt. Ladislaus Chang’a wakati wa uzinduzi wa mradi wa ‘HIGH impact Weather lAke sYstem (HIGHWAY)’ uliofanyika katika ukumbi wa Ubungo Plaza jijini Darves Salaam.

‘Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imedhamiria kuongeza ufanisi wa uandaaji na usambazaji kwa wakati wa taarifa za hali ya hewa hususani taarifa za hali mbaya ya hewa kwa watumiaji wa Ziwa Victoria" amebainisha Dkt. Chang’a.

Ameongeza kuwa, wadau wa mradi huu wakiwemo wataalam kutoka TMA watakaa kwa pamoja na kufanyia maboresho taarifa zinazotolewa na Mamlaka na hivyo kufanikisha utoaji wa huduma bora zaidi zitakazoweza kusaidia serikali katika jitihada za kuhakikisha huduma za hali ya hewa nchini zinachangia katika kufanikisha mikakati na jitihada za nchi kufikia uchumi wa kati na uchumi wa viwanda , ‘

Mapema katika ufunguzi, huo Rita Roberts mtaalam wa mradi kutoka ‘National Centre for Atmosphere Research (NCRA)’ alifafanua kuwa mradi huo utasaidia Kanda ya Afrika Mashariki kupitia taasisi zake za hali ya hewa kufanikisha utoaji endelevu wa tahadhari za hali mbaya ya hewa kwa wakati pamoja na kuongeza kiwango cha usahihi na uhakika kwa taarifa za hali ya hewa na hivyo kupunguza athari za vifo na upotevu wa mali.

Mradi huu unahusisha Taasisi za Hali ya Hewa za Tanzania, Kenya, Uganda na Rwanda kwa kushirikiana na Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) na ‘National Centre for Atmosphere Research (NCRA)’ kutoka Marekani, Taasis ya Hali ya Hewa ya Uingereza (UKMet Office) kwa ufadhili wa ‘Department for International Development (DFID)’ ya Uingereza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...