WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (katikati) akiwa na Mbunge wa Jimbo la Ilala, Mussa Azan Zungu (kulia), wakiwasaka watumia dawa za kulevya (mateja) ambao wanafanya matukio ya uhalifu katika Bonde la Jangwani, Ilala, Jijini Dar es Salaam. Lugola alimpa saa nne Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, kuwakamata wahalifu hao na ifikapo muda huo atafika kituo cha Polisi Msimbazi kwa ajili ya kuwaona watuhumiwa hao. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto), akimsalimia Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, ACP Zuberi Chembera, alipompigia simu afike katika eneo la Bonde la Msimbazi, kuongeza kasi ya kuwasaka watumia dawa za kulevya (mateja) ambao wanatuhumiwa kufanya matukio ya ukabaji, na upora wa mali za watu mbalimbali katika eneo hilo. 
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (watatu kulia) akiwa na Mbunge wa Jimbo la Ilala, Mussa Azan Zungu (wapili kulia), wakiwasaka watumia dawa za kulevya (mateja) ambao wanafanya matukio ya uhalifu katika Bonde la Jangwani, Ilala, Jijini Dar es Salaam. Lugola alimpa saa nne Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, kuwakamata wahalifu hao na ifikapo muda huo atafika kituo cha Polisi Msimbazi kwa ajili ya kuwaona watuhumiwa hao. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 



Na Felix Mwagara, MOHA. 

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, amefanya operesheni ya kuwasaka na kuwakamata mateja mbalimbali ambao wanatumia dawa za kulenya na kufanya uhalifu katika bonde la Jangwani, Ilala, jijini Dar es Salaam. 

Lugola ambaye aliongozana na Mbunge wa Jimbo la Ilala, Mussa Azan Zungu, kuwasaka mateja hao ambao wanatumia aina mbalimbali ya madawa ya kulenya, baada ya kuona viongozi hao wanawasaka walikimbia katika maeneo ya vijiwe vyao. 

Waziri Lugola wakati akiwa katika operesheni hiyo ambayo ilidumu kwa saa moja na nusu kwa kutembelea mitaa mbalimbali ya bonde hilo, alimpigia Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala-RPC, ACP Zuberi Chembera, kufika katika eneo hilo huku akiwa na askari kwa ajili ya kuendeleza zoezi hilo. 

Akizungumza na wananchi wa Kata hiyo ya Jangwani, leo, Waziri Lugola alisema wahalifu hawa wanapaswa kusakwa kwa nguvu zote na kukamatwa, kwasababu walishampora mtu katika mitaa hiyo na kumuaa. 

“RPC kuanzia muda huu, nakuagiza askari wako waingie mitaani, kuwakamata wahalifu hawa, na nitakuja saa 12 jioni ya leo, kuona wahalifu wote katika bonde hili wamejaa katika kituo cha Msimbazi, na muwakamate wahalifu na sio kuwaonea watu wasiokuwa na makossa,” alisema Lugola. 

Lugola aliongeza kuwa, Serikali haiwezi kukaa kimya kufumbia macho matukio ya kiuhalifu ambayo yamekithiri katika eneo hilo na kuwafanya wananchi kutopata usingizi kuhofia kuvamiwa kwa muda wowote usiku au mchana. Alimtaka Kamanda wa Polisi Mkoa huo, kuendelea kufanya operesheni ya mara kwa mara kuwasaka wahalifu hao ambao wengi wao ni mateja ambao wanatumia dawa za kulevya. 

Kwa upande wake Mbunge Zunge, ambaye ndio alimwita Waziri huyo kutembelea eneo hilo kuona kero kubwa awanazopata wananchi wake, alisema wahalifu hao hawatoki pekee katika Jimbo lake, bali wengi wao wanatoka maeneo mbalimbali katika Jiji la Dar es Salaam. 

“Wenyeji wa eneo hili ni wachache, wengi wanatoka mitaa mbalimbali ya hapa Dar es Salaam ikiwemo Temeke na kwingineko, hivyo mheshimiwa Waziri tunajua utendaji wako, tunakuomba hii kero inatuumiza sana, wananchi wanakosa amani kutokana na uwepo mkubwa wa wahalifu hawa,’ alisema Zungu. 

Waziri Lugola alisema Dkt John Magufuli anawataka wananchi wake waishi kwa amani na utulifu, yeye Waziri hatakubali kuona matukio hayo ya baibu yakishika kasi mitaani. Aliwataka Makamanda wa Polisi nchini kuwasaka wahalifu muda wowote si mpaka yeye atoe agizo au atembeleee.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...