Leandra Gabriel na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.
BIASHARA ya utumwa ilikuwa biashara iliyodhalilisha utu wa binadamu, hasa Waafrika ambao ndio waliotumika kwa kiasi kikubwa katika biashara hiyo. 

Baadhi ya watu Ulaya waliweza kuona madhara mbalimbali yaliyotokana na biashara hiyo hatarishi, na kuamua kuanzisha tapo la kuikomesha. Wengi wao walikuwa watu wa dini waliosukumwa na sababu za ubinadamu.

Ikiwa leo ni siku ya kumbukumbu ya biashara ya utumwa duniani kote ambayo huadhimishwa kila ifikapo Agosti 23 kila mwaka ili kukomesha biashara hiyo. Nasi kama Tanzania biashara ya watumwa ilikuwepo huko Bagamoyo na maeneo mbalimbali ambapo wanunuzi wa bianadamu walikuwa wakiwanunua binadamu wenzao kwajili ya kuwatumikisha katika kazi.

Baadaye mataifa kama Uingereza yaliongeza bidii katika ukomeshaji wa biashara ya utumwa, kwa kiasi fulani ukomeshaji wa biashara ya utumwa ulikuwa una manufaa ya kiuchumi kwao, hasa kufuatia matokeo ya mapinduzi ya viwanda yaliyotokea.
Usiku wa tarehe 22 na 23 Agosti mwaka 1971 huko Santo Domingo na Haiti kama ijulikanavyo kwa sasa mwanzo wa kukomesha biashara ya utumwa ile ya kupitia bahari ya Atlantic (Transatlantic slave trade) ulianza.

Kutokana na kupingwa kwake ikatengwa siku maalumu ya kukumbuka kwa kila mwaka na siku hii ya Agosti 23 imelenga kukumbuka huzuni iliyotokana na biashara ya utumwa kwa watu wote.

Mkurugenzi mtendaji wa shirika la elimu, sayansi na teknolojia (UNESCO) Audrey Azoulay, ametoa ujumbe katika siku hii adhimu kwa kuwaalika mawaziri wenye dhamana ya utamaduni katika nchi zote wanachama kuadhimisha Agosti 23, kila mwaka kwa kuwashirikisha wananchi, vijana, wasanii na wataalamu mbalimbali.

Kupitia ujumbe wake ameeleza kuwa siku ya kukumbuka biashara ya utumwa na kukomeshwa kwake kwa mara ya kwanza iliidhinishwa na nchi nyingi zikiwemo Haiti (Agosti 23, 1998) na Goree Senegal (23 Agosti 1999) na matukio mbalimbali ya kitamaduni na midahalo ilifanyika.

Mwaka 2001 Makumbusho ya Mulhouse Textile ya huko Ufaransa walishiriki kwa kuandaa maonesho yaliyojulikana "Indiannes de Traite"

Ili kuendelea kufunza vizazi kuhusiana na biashara hiyo waziri wa utamaduni anawaalika nchi wanachama kuadhimisha siku hiyo kila mwaka katika nchi zao kwa kuandaa midahalo ya wazi na tafiti zilizofanywa na wananchi wa kawaida ili kuinua uelewa kuhusiana na historia tuliyopiyia na kupinga kila aina ya utumwa wa kisasa.

Katika kukumbuka siku hiyo imeelezwa lazima masuala ya ukusanyaji wa taarifa yatupiwe macho na hiyo ni kupitia misafara ya watumwa kwa kuangalia sababu za kihistoria zilizosababisha, njia walizotumia pamoja na matokeo ya biashara hiyo ambayo iliunganisha mabara ya Ulaya, Afrika, Amerika na Caribbean.

Hata hivyo Uingereza ikiwa taifa kiongozi katika biashara hiyo, halafu katika zoezi hilo la kuikomesha, ulisaidia kwa kiasi kikubwa katika ukomeshaji wa biashara hii iliyopitia katika bahari ya Atlantiki na ile ya bahari ya Hindi.

Si mataifa yote yalikubaliana na matakwa ya Uingereza ya kukomesha biashara ya utumwa, hivyo Uingereza ilipata upinzani kutoka kwa mataifa mengine yaliyokuwa bado yananufaika na biashara hii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...